Wanachama wa WHO wakaribisha Palestina kupatiwa haki sawa za uanachama
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i112494-wanachama_wa_who_wakaribisha_palestina_kupatiwa_haki_sawa_za_uanachama
Nchi za wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO) zimekubaliana na suala la Palestina kupatiwa haki sawa za uanachama katika shirika hilo la kimataifa.
(last modified 2026-07-02T04:13:23+00:00 )
Jun 03, 2024 03:23 UTC
  • Wanachama wa WHO wakaribisha Palestina kupatiwa haki sawa za uanachama

Nchi za wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO) zimekubaliana na suala la Palestina kupatiwa haki sawa za uanachama katika shirika hilo la kimataifa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la (ISNA); kwa mara ya kwanza katika historia ya mikutano ya Baraza la Shirika la Afya Ulimwenguni kulitengwa kiti cha Palestina kwa mpangilio wa alfabeti huku kukiwa na shangwe za wawakilishi wa nchi waliohudhuria wakati wa kufunga mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la WHO.

Inakaribisha utoaji wa haki sawa za uanachama kwa Palestina katika Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO)

Katika kikao cha mwisho cha Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Shiriika la Afya Duniani huko Geneva, Jumamosi ya juzi, nchi za wanachama wa WHO zilikubaliana kwa wingi wa kura kutoa haki sawa ya uanachama kwa Palestina kwa ajili ya kuwaunga mkono watu wa Ukanda wa Gaza wanaouawa kila siku.

 Wiki hii, wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO) katika muktadha wa mkutano wa shirika hilo la kimataifa kama chombo cha juu zaidi cha maamuzi walipiga kura ya kuunga mkono rasimu ya azimio kwa lengo la kutekeleza ushiriki wa Palestina.

Katika rasimu hiyo, iliyowasilishwa na kundi la nchi za Kiarabu na Kiislamu, pamoja na China, Nicaragua na Venezuela, iilitaka Wapalestina ambao ni wanachama waangalizi wa Shirika la Afya Duniani wapewe takriban haki sawa na wanachama kamili.

Kura hiyo mjini Geneva ilikuja baada ya wajumbe wengi wa Umoja wa Mataifa (UN) kupiga kura mjini New York mwezi Mei ili kutoa haki zaidi kwa Wapalestina katika taasisi hiyo licha ya njama za nchi za Marekani na Magharibi kuzuia uanachama kamili wa Palestina katika Umoja wa Mataifa.