Jeshi la Yemen lashambulia meli ya kivita ya Uingereza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i112754-jeshi_la_yemen_lashambulia_meli_ya_kivita_ya_uingereza
Vikosi vya wanamaji vya Yemen vimefanya operesheni mbili tofauti dhidi ya meli ya kivita ya Uingereza na pia meli mbili za kibiashara katika pwani ya taifa hilo ikiwa ni hatua ya kuonyesha mshikamano na Wapalestina wa Gaza ambao wanakabiliwa na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel kwa himaya ya Marekani na Uingereza.
(last modified 2024-06-10T01:19:02+00:00 )
Jun 10, 2024 01:19 UTC
  • Jeshi la Yemen lashambulia meli ya kivita ya Uingereza

Vikosi vya wanamaji vya Yemen vimefanya operesheni mbili tofauti dhidi ya meli ya kivita ya Uingereza na pia meli mbili za kibiashara katika pwani ya taifa hilo ikiwa ni hatua ya kuonyesha mshikamano na Wapalestina wa Gaza ambao wanakabiliwa na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel kwa himaya ya Marekani na Uingereza.

Jeshi la Yemen lilitangaza katika taarifa siku ya Jumapili kwamba vikosi hivyo viliilenga meli ya kivita ya Uingereza ijulikanayo kama HMS Diamond katika Bahari ya Sham kwa makombora ya balestiki, na kusisitiza kwamba shambulio hilo lilikuwa "sahihi."

Jeshi la Yemen pia limebainisha kuwa vikosi vyake vya wanamanji pia vimeshambulia meli mbili za kibiashara ambazo ilizitaja kuwa ni Norderney na Tavvishi zinazofanya biashara na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Wananchi wa Yemen wametangaza uungaji mkono wao wa wazi kwa mapambano ya Palestina dhidi ya utawala ghasibu wa Israel tangu utawala huo ghasibu ulipoanzisha vita vikali dhidi ya Gaza tarehe 7 Oktoba.

Vikosi vya Wanajeshi wa Yemen vimesema kwamba havitasimamisha mashambulizi yao hadi Israel isitishe mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza ambayo hadi sasa yamesababisha vifo vya Wapalestina takriban 37,100 na kuwajeruhi wengine 84,500, wengi wakiwa ni wanawake na watoto.

Kombora la Jeshi la Yemen la Qaher

Hivi karibuni Jeshi la Yemen lilishambulia kwa mafanikio meli kubwa ya kivita ya Marekani yenye uwezo wa kusheheni ndege ijulikanayo kama USS Eisenhower na kuilazimu kuondoka karibu na pwani ya Yemen.

Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yeme Abdul-Malik al-Houthi amesema ni "heshima na baraka kubwa kukabiliana na Marekani moja kwa moja."

Mashambulizi hayo yamelazimisha baadhi ya makampuni makubwa zaidi ya meli za mizigo na mafuta duniani kusimamisha usafiri kupitia mojawapo ya njia muhimu zaidi za biashara ya baharini katika Bahari ya Sham. Badala yake Meli sasa zinalazimika kuzunguka bara la Afrika badala ya kupitia Mfereji wa Suez.