Sinwar: Tuko tayari kufanya mazungumzo iwapo vita vya Gaza vitasitishwa
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa kushiriki kwao katika mazungumzo ya Doha kunategemea na kusimamishwa vita katika Ukanda wa Gaza.
Yahya Sinwar Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ametuma ujumbe kwa ajili ya usuluhishi na akasema utawala wa Kizyauni unapasa kusitisha harakati zake za kijeshi katika Ukanda wa Gaza kama kweli uko jadi katika mazungumzo na unataka kufikiwa mapatano.
Kuhusiana na suala hilo, Shirika la habari la Reuters awali liliinukuu duru moja ya harakati ya Hamas na kuripoti kuwa wawakilishi wa harakati hiyo hawatashiriki katika mazungumzo ya kesho huko Doha,Qatar. Misri, Qatar na Marekani ambazo ni pande suluhishi katika mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Hamas na utawala bandia wa Israel hivi karibuni zilitoa taarifa zikizialika Hamas na utawala wa kizayuni katika mazungumzo ya kusimamisha vita yaliyopangwa kufanyika kesho huko Doha, Qatar.
Hamas Jumapili usiku wiki hii ilitoa taarifa ikisisitiza kuwa vipengee vilivyofikiwa katika mapatano ya awali vinapasa kutekelezwa kwanza badala ya kuanza mazungumzo mapya ya kusimamisha vita huko Gaza na amezitaka pande suluhushi kuja na mpango kwa mujibu wa mazungumzo ya awali.