UNRWA yatahadharisha kuhusu vifo vya raia katika Ukanda wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i115516-unrwa_yatahadharisha_kuhusu_vifo_vya_raia_katika_ukanda_wa_gaza
Afisa mmoja wa UNRWA ametahadharisha kuhusu kuendelea mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na kusema: Vifo ni hatima pekee inayowakabili watu wa Gaza na kuwa hakuna njia nyingine ya kuepuka jinai zisizo na kikomo za utawala huo.
(last modified 2024-08-22T08:26:14+00:00 )
Aug 22, 2024 08:26 UTC
  • UNRWA yatahadharisha kuhusu vifo vya raia katika Ukanda wa Gaza

Afisa mmoja wa UNRWA ametahadharisha kuhusu kuendelea mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na kusema: Vifo ni hatima pekee inayowakabili watu wa Gaza na kuwa hakuna njia nyingine ya kuepuka jinai zisizo na kikomo za utawala huo.

Shirika la habari la ISNA limeripoti kuwa,  Louise Waterridge, Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada kwa ajili ya Wakimbizi wa Palestina (UNRWA), ameeleza kuwa "Katika miezi miwili iliyopita, kumekuwa na mgogoro wa binadamu katika Ukanda wa Gaza, hofu ya watu kuuawa na kuenea magonjwa wakati huu ambapo utawala wa Kizayuni unaendeleza vita na mauji ya kimbari dhidi ya wakazi wa eneo hilo.  

Waterridge pia amesisitiza kuhusu kambi ya al Nuseirat inayopatikana katikati ya Ukanda wa Gaza ambayo ni moja ya maeneo yanayokabiliwa na mashambulizi ya anga ya jeshi la Israel na kwamba hakuna eneo lililo salama katika kambi hiyo na hali ni ya kuhuzunisha sana.  

Mauaji ya kimbari ya Israel katika kambi ya al Nuseirat 

Msemaji wa shirika la UNRWA amesisitiza kuwa hakuna shule hata moja katika Ukanda wa Gaza inayochukuliwa kuwa mahali salama, na watu wengi wamelazimika kuhamia katika sehemu zisizojulikana katika Ukanda huo na kwamba ni wazi kuwa raia hao wanafuatiliwa na kusakwa na wanajeshi wa Israel.