Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen: Yahya Sinwar alikuwa na mchango muhimu katika vita dhidi ya Israel
(last modified 2024-10-21T02:48:06+00:00 )
Oct 21, 2024 02:48 UTC
  • Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen: Yahya Sinwar alikuwa na mchango muhimu katika vita dhidi ya Israel

Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen ameeleza kuwa shahidi Yahya Sinwar Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Hamas alikuwa na mchango muhimu katika vita nan utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na ndio maana akawa shabaha ya utawala wa Kizayuni na kuuliwa shahidi.

Yahya al Sinwar Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) aliuawa shahidi Jumatano iliyopita akipambanana adui Mzayuni katika mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza. Ya

Shahidi Yahya Sinwar 

Jamal Amir Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen amefanya mahojiano maalumu na shirika la habari ya Iran Press huko Sana'a mji mkuu wa Yemen na kusema kuuliwa shahidi Yahya Sinwar akiwa mstari wa mbele katika medani ya vita ya muqawama mkabala wa Israel ni sawa na kushindwa utawala huo. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen amesisitiza kuwa, kuuliwa shahidi al Sinwar akipigana vita dhidi ya Wazayuni huko Ukanda wa Gaza kuonyesha nguvu na azma thabiti ya wanamuqawama kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya ukombozi dhidi ya adui Mzayuni.