Jarida la Marekani, Foreign Affairs: Hamas itabakia hai
(last modified Wed, 23 Oct 2024 02:26:09 GMT )
Oct 23, 2024 02:26 UTC
  • Jarida la Marekani, Foreign Affairs: Hamas itabakia hai

Jarida la Marekani la "Foreign Affairs" limeandika katika ripoti yake kwamba, kuuawa shahidi Yahya al-Sinwar, sio tu kwamba hakutaiangamiza Hamas, bali Harakati hiyo ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina itaendelea kufanya kazi zake za mapambano ya ukombozi.

Yahya al-Sinwar, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) aliuawa shahidi siku ya Jumatano (16 Oktoba) akipigana na wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel katika mji wa Rafah (kusini mwa Ukanda wa Gaza).

Likizungumzia tukio la kuuawa shahidi kiongozi wa Hamas, Yahya Sinwar, jarida la Marekani la Foreign Affairs limeandika kwamba: "Israel imekuwa ikiwaua kigaidi viongozi wa Hamas kwa miongo kadhaa; Kama Hamas ingeathiriwa na mkakati huu, basi ingedhoofika na kuangamizwa kwa mauaji ya watu kama vile Yahya Ayyash, Sheikh Ahmed Yassin, Abdulaziz Rantisi, na katika vita vya sasa kwa mauaji ya Saleh al-Arouri, Marwan Issa na Ismail Haniyeh.Hamas

Jarida la Marekani la Foreign Affairs limesisitiza kuwa, Israel lazima ikubali kwamba sera ya kuwaua viongozi wa Hamas ili kudhoofisha harakati hiyo imeshindwa na kufeli.

Jarida hilo pia limeeleza kwamba, licha ya kuuawa shahidi Yahya Sinwar, Hamas inaendelea kushikilia stratijia yake ya mapambano na muqawama hadi ardhi na maeneo matakatifu ya Palestina yatakapokombolewa, na kuongeza kuwa, kutokana na mauaji ya Sinwar, Sinwar wengi huko Gaza wanataka kulipiza kisasi kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Tags