Jul 27, 2016 04:00 UTC
  • Magaidi 120 wa Daesh wauawa Afghanistan

Makumi ya wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh wameuawa katika operesheni kali ya jeshi la Afghanistan, katika mkoa wa Nangarhar, kaskzini mwa nchi.

Attaullah Khogyani, msemaji wa mkoa huo amesema magaidi hao wameangamizwa katika operesheni hiyo iliyoonekana kuwa ya ulipizaji kisasi, siku mbili baada ya magaidi hao kuua idadi kubwa ya waandamanaji katika mji mkuu Kabul. Mohammad Radmanish, msemaji wa jeshi la nchi hiyo amethibitisha kutokea operesheni hiyo na kusistiza kuwa, vyombo vya usalama vimeazimia kulitokomeza kikamilifu kundi hilo la kitakiri.

Athari za shambulio la kigaidi katika mji wa Kabul Julai 23

Haya yanajiri siku tatu baada ya watu 80 kuuawa na wengine 300 kujeruhiwa katika hujuma ya kigaidi Jumamosi iliyopita katika mji wa Kabul. Shambulio hilo lilitokea wakati maelfu ya wananchi walipokuwa wakiandamana kulalamikia mradi wa umeme uliozusha mjadala mkubwa, kutoka nchini Turkmenistan kupitia njia ya eneo la milima ya Salang, badala ya maeneo ya wanavijiji.

Rais Ashraf Ghani wa Afghanistan akisisitiza jambo

Rais Ashraf Ghani mbali na kusisitiza kuwa wahusika wa shambulio hilo la kigaidi wanakusudia kuibua mpasuko na fitina katika jamii na watu wa nchi hiyo, amesema kamwe magaidi hao hawatofikia malengo yao machafu.

Tags