Wazayuni 3 waangamizwa katika oparesheni ya Ukingo wa Magharibi
Duru za habari zimearifu kuwa Wazayuni watatu wameangamizwa katika oparesheni iliyofanywa dhidi ya wavamiizi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan.
Vyombo vya habari vya Israel vimetangaza kuwa mtu mmoja aliyekuwa ndani ya gari karibu na kijiji cha al Funduq mashariki mwa Qalqiliya katika Ukingo wa Magharibi alilifyatulia risasi basi la Wazayuni na kuwaangamiza watatu miongoni mwao.
Televisheni ya utawala wa Kizayuni imetangaza kuwa hadi kufikia sasa Wazayuni watatu wameangamia na wengine sita kujeruhiwa; huku hali ya majeruhi watatu ikiwa mbaya.
Imeelezwa kuwa gari hilo lilikuwa na watu kadhaa na walikuwa wakielekea Nablus.
Jumamosi wiki hii pia walowezi kadhaa wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan walishambuliwa kwa risasi. Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema kuwa ufyatuaji risasi huo ni jibu la kawaida kwa vita na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.
Hamas imetangaza kuwa oparesheni dhidi adui Mzayuni zitaongezeka katika siku zijazo.