Gazeti la Kizayuni lakiri, makombora ya Wayemeni ni hatari
Gazeti la Kizayuni la Jerusalem Post limekiri kuwa makombora ya Yemen yana uwezo wa hali ya juu.
Gazeti hilo la Israel limeandika kuwa vita vya kisaikolojia vya Wayemeni vinadhoofisha uhusiano kati ya wananchi na viongozi wa Israel, na jibu la haraka la jeshi la Yemen kwa kuvurumisha makombora baada ya mashambulizi ya Israel na Marekani huko Yemen linabeba ujumbe kwamba bado wako imara na wana uwezo usiotetereka.
Jerusalem Poost limeongeza kuwa, makombora ya Yemen yanayovurumishwa dhidi ya Israel yana malengo ya kijeshi na kisaikolojia, pia na ysmsvuruga hali ya usalama yan Israel na washirika wake.
Jeshi la Yemen, mwaka mmoja uliopita na katika kuunga mkono mapambano ya wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza, limekuwa likishambulia mara kadhaa meli za Wazayuni au zile zinazoelekea katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) katika Bahari Nyekundu na Mlango Bahari wa Babul Mandab .
Jeshi la Yemen pia limetekeleza mashambulizi kadhaa ya makombora na ndege zisizo na rubani kwenye ardhi zinazokaliwa kwa mabavu hasa mji wa Tel Aviv na kuahidi kuwa litaendelea kuzishambulia meli na maeneo mbalimbali ya utawala wa kizayuni madhali Israel inaendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Gaza.