Sep 01, 2016 03:54 UTC
  • Wanazuoni wawili wa Kishia wa Saudia watiwa mbaroni Makka

Askari usalama wa Saudi Arabia wamewatia mbaroni wanazuoni wawili wa Kishia wa nchini humo.

Habari zinasema kuwa askari usalama wa Saudia leo wametia mbaroni wanazuoni wawili wa Waislamu wa madhehebu ya Shia kwa majina ya Sheikh Muhammad Zainulddin na Sayyid Jaafar Alawi, wakazi wa mji wa Qatif kwa visizingizio visivyo na msingi.

Askari usalama wa utawala wa Aal Saud wamekuwa wakiwatia mbaroni kiholela wanaharakati wa kisiasa na wa kidini huko Saudia.

Kabla ya hapo pia Idara ya Mahakama ya utawala wa Aal Saud ilitekeleza hukumu ya kunyongwa Sheikh Nimr Baqir al Nimr mwanazuoni mtajika wa Saudia hatua iliyokosolewa na kulalamikiwa pakubwa na duru za ndani, kieneo na kimataifa.

Maeneo ya Qatif huko mashariki mwa Saudi Arabia yamekuwa yakishuhudia maandamano na upinzani wa wananchi dhidi ya dhulma na jinai zinazofanywa na utawala wa Aal Saud; maandamano ambayo hata hivyo yamekuwa yakikandamizwa na askari usalama wa nchi hiyo.

Maandamano ya wananchi katika mji wa Qatif kupinga utawala wa Aal Saud

 

Tags