'Kusimama kidete Syria ni katika heshima za umma wa Kiislamu'
-
Rais Bashar al Assad wa Syria
Mwanaharakati mmoja wa Misri amesema kuwa, Syria ni katika mataifa ya kujivunia ya ulimwengu wa Kiislamu na kujilinda na kusimama kidete nchi hiyo ni heshima kwa umma wa Kiislamu.
Bi Shaima Ahmad msemaji wa chama cha al Tadhamun ameliambia shirika la habari la Fars kwamba, siasa za mambo ya ndani na mambo ya nje za Marekani zimejaa uongo na ulaghai kuhusiana na masuala ya uhuru na demokrasia. Amesema, kusimama kidete Syria kukabiliana na njama za madola ya kibeberu kunafanyika kwa ajili ya kulinda heshima ya umma mzima wa Kiislamu.
Mwanaharakati huyo ameongeza kuwa, Marekani ni nchi inayoeneza propaganda za uongozo na kusisitiza kuwa, nchi hiyo haiwezi kuweka wazi malengo yake ya kweli na kwamba siasa za ndani na nje za Marekani zimegubikwa na uongo na ulaghai.
Bi Shaima Ahmad ameongeza kuwa, nchi ambayo imeundwa kwa msingi wa kupotosha historia na kuvamia ardhi ya watu wengine na kufanya mauaji ya umati na kukiangamiza kizazi kizima cha Wahindi Wekundu, kamwe haiwezi kuwa nchi yenye haki na uadilifu.
Mwanaharakati huyo wa Misri ameongeza kuwa, uhuru nchini Marekani si zaidi ya sanamu maarufu ambalo linaakisi jinai za Wamarekani dhidi ya Wahindi Wekundu, dhidi ya jamii za watu wachache na dhidi ya mataifa yote mengine duniani.
Vile vile amegusia njama za Marekani za kutaka kuwadhibiti na kuwafanyia ubeberu watu wote duniani na si kupigania haki na kusema kuwa, lengo la Marekani ni kupora utajiri wa nchi nyingine na kufanikisha malengo ya Uzayuni wa kimataifa, si jambo jingine lolote.