Marekani yakiri kuua makumi ya raia Iraq na Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i20575-marekani_yakiri_kuua_makumi_ya_raia_iraq_na_syria
Jeshi la Marekani limetoa taarifa na kukiri kuwa, muungano unaodaiwa kupambana na genge la kigaidi la Daesh unaoongozwa na Washington umeua makumi ya raia katika kipindi cha tarehe 31 Machi hadi 22 Oktoba mwaka huu huko Iraq na Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 02, 2016 00:51 UTC
  • Marekani yakiri kuua makumi ya raia Iraq na Syria

Jeshi la Marekani limetoa taarifa na kukiri kuwa, muungano unaodaiwa kupambana na genge la kigaidi la Daesh unaoongozwa na Washington umeua makumi ya raia katika kipindi cha tarehe 31 Machi hadi 22 Oktoba mwaka huu huko Iraq na Syria.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, raia 24 waliuwa mwezi Julai tena katika shambulio moja tu lililofanywa na muungano huo kaskazini mwa Syria.

Muungano huo unoongozwa na Marekani umekiri pia kuwa, zaidi ya raia 170 wameuliwa kwenye mashambulizi yanayodaiwa ni ya kupambana na genge la wakufurishaji la Daesh, yanayoongozwa na Marekani nchini Syria na Iraq.

Taarifa zisizo rasmi zinaonesha kuwa, mauaji ya raia yanayofanywa na muungano unaoongozwa na Marekani huko Syria na Iraq ni makubwa mno kuliko hayo yanayotangazwa na jeshi la Marekani.

Wananchi wa Syria wakikimbilia maeneo yenye usalama yaliyoko mikononi mwa jeshi la nchi hiyo.

 

Hii ni katika hali ambayo hadi hivi sasa muungano huo umeshindwa kupata mafanikio yoyote ya maana katika madai yake ya kupambana na Daesh.

Muungano huo unafanya mashambulizi nchini Syria bila ya idhini ya serikali halali ya nchi hiyo na bila ya kibali cha Umoja wa Mataifa.

Marekani na kundi lake wanadai kupambana na magaidi wa Daesh katika hali ambayo baadhi ya ripoti zinaonesha kuwa, Marekani na Saudi Arabia zilikubaliana kuwahamisha magaidi wa Daesh kutoka Mosul Iraq na kuwapeleka mashariki mwa Syria.