Apr 14, 2017 07:47 UTC
  • Israel yaamuru kubomolewa Msikiti Ukingo wa Magharibi

Utawala haramu wa Israel umetoa amri ya kubomolewa msikiti katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la Quds Mashariki kwa madai kwamba msikiti huo ulijengwa bila ya kupata vibali.

Amri ya kubomolewa Msikiti wa Abdullah al Sanawi ilitolewa jana Alhamisi na serikali ya utawala haramu wa Israel. Mjumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Silwan, Fakhri Abu Diab amesema msikiti huo ulijengwa miaka kadhaa iliyopita katika ardhi ya waqfu kwa kutumia fedha za michango ya wananchi na unatoa huduma kwa wakazi 4000 wa eneo hilo. Msikiti wa Abdullah Al Sanawi ni kati ya misikiti 6 ya Wapalestina iliyotishiwa kubomolewa na mamlaka za utawala haramu wa Israel. 

Disemba mwaka jana ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu (OCHA) ilitangaza kuwa wimbi la bomoabomoa ya Israel dhidi ya nyumba na miundombinu ya Wapalestina katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi na Quds  Mashariki limefikia kiwango ambacho hakijawahi kuhushudiwa katika miaka kadhaa iliyopita. 

Tags