Oct 06, 2024 11:06 UTC
  • Unicef: Watoto zaidi ya 100 wameuawa Lebanon katika siku 11

Mfuko wa Kuwahudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (Unicef) umetangaza kuwa watoto zaidi ya 100 wameuawa huko Lebanon siku 11 zilizopita kufuatia hujuma na mashambulizi yanayoendelea kufanywa na jeshi la Israel nchini humo.

Shirika la Unicef limetangaza taarifa hii katika ujumbe wake uliotumwa katika mtandao wa X likitilia mkazo jitihada za kutoa misada ya dharura ya kimatibabu na huduma muhimu kwa watu walioathiriwa na mashambulizi ya Israel huko Lebanon. 

Unicef imesema, watoto zaidi ya 690 wamejeruhiwa katika muda wa wiki sita za mashambulizi na mauaji yanayoendelea kufanywa na jeshi la Israel huko Lebanon. 

Hujuma za Israel huko Lebanon 

Tangu Septemba 23, Israel imepanua mauaji ya kimbari katika maeneo mbalimbali ya Lebanon ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa nchi hiyo, Beirut baada ya mauaji ya kimbati ya karibu mwaka mzima katika eneo la Ukanda wa Gaza.

"Mashambulizi hayo yanajumuisha mashambulizi ya anga yanayotekelezwa na ndege za kivita za Israel ambayo hayajawahi kushuhudiwa na pia mashambulizi ya nchi kavu kusini mwa Lebanon, licha ya indhari za kimataifa na maazimio ya Umoja wa Mataifa", imesema taarifa ya Unicef. 

Tags