Oct 08, 2017 07:50 UTC
  • Waisraeli waandamana Tel Aviv dhidi ya ufisadi wa Netanyahu

Wakazi wa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu utawala wa Kizayuni wameandamana huko Tel Aviv wakitaka kushughulikiwa kesi ya ufisadi inayomkabili Waziri Mkuu wa utawala huo ghasibu.

Waisraili jana usiku walifanya maandamano mjini Tel Aviv mbele ya nyumba ya Avichai Mandelblit, Mshauri wa Masuala ya Sheria wa Serikali ya Israel mashariki mwa mji huo. Waandamanaji wametaka kuchukuliwe hatua haraka iwezekanavyo ili kumaliza kesi hiyo ya ufisadi inayomkabili Benjamin Netanyahu  na wametaka kutangazwa matokeo yake haraka iwezekanavyo. 

Maandamano ya kutaka kumuondoa madarakani Netanyahu na kuharakishwa uchunguzi dhidi yake yalianza miezi kadhaa iliyopita mjini Tel Aviv na katika maeneo mengine ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu; na yanaendelea hadi sasa.

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni anayekabiliwa na kesi ya ufisadi  

Uchunguzi kuhusu tuhuma za ufisadi na kupokea rushwa ya mamilioni ya dola kutoka kampuni moja ya Ujerumani zinazomkabili Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni ulianza tangu Januari Pili mwaka huu. Kesi ya msingi inayomkabili Netanyahu inahusiana na kupokea kiasi cha dola milioni moja kutoka kwa Arnaud Mimran, fisadi wa uchumi, raia wa Ufaransa ambazo inasemekana kuwa zimetumika katika kumpigia kampeni Netanyahu.  

Tags