Rais Putin awapongeza wanajeshi wa Russia walioko Syria
Rais Vladimir Putin wa Russia amewapongeza na kuwashukuru wanajeshi wa nchi yake walioko nchini Syria.
Kwa mujibu wa televisheni ya Roosiya al Youm, akizungumza katika sherehe ya siku ya 'Wanaounga Mkono Nchi' kwa mara nyingine amewashukuru wanajeshi wote wa Russia wanaohudumu nchini Syria.
Putin ameongeza kuwa, wanajeshi hao wamejitayarisha kikamilifu na kwamba wataendelea na mapambano bila woga hadi mwisho.
Rais wa Russia amesema: "Matukio ya miaka ya hivi karibuni yamethibitisha kuwa, kwa matazamo wa kuwa tayari kijeshi, kiwango cha silaha na suhula za kijeshi, Russia ni kati ya nchi zilisostawi zaidi duniani.
Mgogoro wa Syria ulianza mwaka 2011 wakati magaidi walipoivamia nchini hiyo kwa himaya ya Saudi Arabia, Marekani na waitifaki wao wakiwemo Uingereza na Ufaransa kwa lengo la kubadilisha mlingano wa kieneo kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni wa Israel. Kufuatia hujuma hiyo, Syria iliomba msaada wa Russia na Iran katika kuisaidia kukabiliana na magaidi.