May 29, 2018 01:43 UTC
  • Askari wa Israel wampiga risasi na kumjeruhi vibaya mwanamke kiziwi wa Palestina

Askari polisi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamemmiminia risasi na kumjeruhi vibaya mwanamke asiye na uwezo wa kusikia wa Kipalestina katika mji mtukufu wa Quds unaokaliwa kwa mabavu.

Polisi ya Israel imesema maafisa wake waliamua kumpiga risasi mwanamke huyo katika kijiji cha Pisgat Ze'ev mjini Quds eti kwa kuwa aliambiwa asimame akakataa.

Hata hivyo mashuhuda katika eneo hilo la tukio wamesema mwanamke huyo ni kiziwi na asingeliweza kusikia sauti ya askari katili wa Israel wakimmuamrisha asimame.

Wanajeshi katili wa Israel

Taarifa ya Polisi ya Israel imedai kuwa, mwanamke huyo ambaye alikuwa amevaa mavazi ya staha ya niqabu alitakiwa kusimama lakini akaendelea na safari yake katika eneo la Beit Hanina, na hapo ndipo askari polisi wakaamua kummiminia risasi na kumjeruhi wakidhani kwamba alikuwa amejifunga mada za miripuko.

Hata hivyo askari hao makatili waligundua kuwa mwanamke huyo hakuwa na silaha ya aina yeyote, na baadaye akakimbizwa hospitalini akiwa na majeraha ya risasi mguuni.

Jeshi la utawala haramu wa Israel limekuwa likiwashambulia Wapalestina madhulumu ambao hawajajizatiti kwa silaha, wakiwemo walemavu, wanawake na watoto wadogo.

Tags