Pakistan yaitaka Saudia kujiepusha na hatua yoyote itakayotishia usalama wa eneo
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i56206-pakistan_yaitaka_saudia_kujiepusha_na_hatua_yoyote_itakayotishia_usalama_wa_eneo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan amesema kuwa, nchi hiyo imeitaka Saudi Arabia kuchukua tahadhari kutokana na uamuzi wowote wa haraka ambao unaweza kutishia usalama na amani ya eneo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 23, 2019 23:24 UTC
  • Pakistan yaitaka Saudia kujiepusha na hatua yoyote itakayotishia usalama wa eneo

Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan amesema kuwa, nchi hiyo imeitaka Saudi Arabia kuchukua tahadhari kutokana na uamuzi wowote wa haraka ambao unaweza kutishia usalama na amani ya eneo.

Shah Mehmood Qureshi ambaye ameelekea mjini New York, Marekani kwa ajili ya kushiriki mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema kuwa wakati Imran Khan, Waziri Mkuu wa Pakistan lipofanya safari nchini Saudia, aliitaka Riyadh kujiepusha na uamuzi wowote unaoweza kutishia usalama na uthabiti wa eneo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan ameongeza kuwa katika safari hiyo, Imran Khan alijadiliana kwa kina na Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud pamoja na Mohammad Bin Salman kuhusiana na matukio ya hivi karibuni katika eneo.

Imran Khan, alipokuwa Saudia

Hivi karibuni jeshi la Yemen kwa kushirikiana na kamati za wananchi, lilitekeleza shambulio dhidi ya vituo vya kusafishia mafuta vya Shirika la Mafuta la Saudia ARAMCO kwenye maeneo ya Buqayq na Khurais kwa kutumia ndege 10 zisizo na rubani, shambulizi lililopelekea hitilafu kwenye shughuli za uzalishai mafuta ndani ya nchi hiyo. Baada ya shambulizi hilo Yahya Saree, Msemaji wa Jeshi la Yemen alitoa taarifa akisema kuwa, operesheni hiyo imetekelezwa ikiwa ni katika fremu ya kisheria ya Wayemen katika kujibu jinai za miaka mitano za muungano vamizi wa Saudia dhidi ya taifa la Yemen. Hata hivyo Marekani katika kukariri madai yake yasiyo na msingi wowote dhidi ya Iran, ilidai kuwa Tehran iko nyuma ya mashambulizi hayo ya Wayemen dhidi ya taasisi za mafuta za Saudia, tuhuma ambazo zimetupiliwa mbali na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.