Walowezi wa Kizayuni wavamia tena Msikiti Mtakatifu wa al-Aqswa
Makumi ya walowezi wa Kizayuni wameuvamia tena Msikiti wa al-Aqswa huko Palestina wakisaidiwa na askari wa jeshi la utawala haramu wa Israel na kuuvunjia heshima msikiti huo ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.
Walowezi hao wa Kizayuni baada ya kuingia katika eneo la ndani la msikiti huo mtakatifu walisikika wakipiga nara dhidi ya Uislamu na Waislamu sambamba na kufanya maeasimuu yao ya kidini katika msikiti huo.
Vyombo vya habari vya Palestina vimeripoti kwamba, hujuma na uvamizi huo umefanyika kwa msaada na uungaji mkono wa wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel.
Walowezi hao wa Kizayuni wamevamia msikiti huo na kusaidiwa na wanajeshi wa Israel katika hali ambayo, Waislamu wamezuia kutekeleza ibada zao za kila siku katika msikiti huo kwa kisingizio cha virusi vya Corona.
Dakta Abdallah Maaruf, afisa wa mahusiano ya uma ya Msikiti wa al-Aqswa amekosoa vikali siasa za kibaguzi za Israel dhidi ya Waislamju Wapalestina hasa hatua ya utawala huo ghasibu ya kuwazuiia Waislamu kuingia katika msikiti huo kwa sasa kwa kisingizio cha virusi vya Corona huku walowezi wa Kizayuni wakiruhusiwa kuingia katika msikiti huo.
Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu vinafanyika katika hali ambayo, viongozi wa nchi za Kiarabu na jamii ya kimataifa wameendelea kunyamaza kimya na kutochukua hatua zozote za kukabiliana na vitendo hivyo.
Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.