Jun 12, 2020 07:46 UTC
  • Mapatano ya Washington na Baghdad kuhusu kupunguzwa askari wa Marekani nchini Iraq

Kumefikiwa mapatano ya kupunguzwa askari wa Marekani nchini Iraq. Mapatano hayo yamefikiwa Alhamisi katika mkutano uliofanyika baina ya Abdulkarim Hashemi Mustafa mwakilishi wa serikali ya Iraq na David Hale mwakilishi wa serikali ya Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa,katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na pande mbili baada ya mazungumzo, Marekani haitafuatilia tena mpango wa kuunda kituo cha kudumu cha kijeshi nchini Iraq.

Aidha taarifa hiyo imesema katika kipindi cha miezi ijayo, Marekani itapunguza askari wake walioko Iraq.

Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al Kadhimi amezungumza baada ya taarifa hiyo na kusema pande mbele zimesisitiza kuhusu Marekani kutekeleza ahadi yake ya kuondoa askari wake nchini Iraq.

Maandamano ya Wairaqi dhidi ya Marekani

Ikumbukwe kuwa mnamo Januari 5, 2020, katika kikao kilichohudhuriwa na waziri mkuu wa wakati huo Adel Abdul Mahdi, Bunge la Iraq lilipiga kura ya kutaka askari vamizi wa Marekani waondolewe nchini humo.

Aidha mnamo Januari 25 mamilioni ya wananchi wa Iraq walishiriki katika maandamano dhidi ya Marekani ambapo walitaka wanajeshi wa Marekani waondoke nchini humo.

Tags