Imarati yafanya njama za kubadili utambulisho wa kisiwa cha Socotra
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i62799-imarati_yafanya_njama_za_kubadili_utambulisho_wa_kisiwa_cha_socotra
Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) ambayo umekivamia na kukikalia kwa mabavu kisiwa cha Socotra huko Yemen unafanya mikakati ya kubadili utambulisho wa kisiwa hicho.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Aug 13, 2020 22:28 UTC
  • Imarati yafanya njama za kubadili utambulisho wa kisiwa cha Socotra

Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) ambayo umekivamia na kukikalia kwa mabavu kisiwa cha Socotra huko Yemen unafanya mikakati ya kubadili utambulisho wa kisiwa hicho.

Baadhi ya duru za habari za Yemen katika viwanja vya ndege vya Aden na Sion na bandari za Hadhramaut na Al Mahrah kusini mwa Yemen zimetangaza kuwa, Imarati imeimarisha hatua kali dhidi ya raia wa Yemen wanaofanya safari kwenye kisiwa hicho na haiwaruhusu kuelekea katika viwanja vya ndege vya Aden na Seun. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, baadhi ya wananchi wa Yemen wanataka kwenda katika kisiwa cha Socotra kwa ajili ya kutalii na wengine kwa ajili ya kufanya biashara, lakini Imarati imewawekea vizuizi vikubwa. 

Kisiwa cha Socotra huko kusini mwa Yemen  

Umoja wa Falme za Kiarabu pia imefukuza idadi kubwa ya wafanyakazi wa Kiyemeni waliokuwa wakifanya kazi katika kisiwa hicho na imetishia kuwafukuza wakazi wengine wa kisiwa hicho. 

Kisiwa cha Socotra huko kusini mwa Yemen mwezi uliopita kilikaliwa na wanajeshi wa Imarati baada ya kushtadi mapigano kati ya wanajeshi wa serikali iliyojiuzulu ya Yemen ya Abdu Rabb Mansour Hadi wanaoungwa mkono na Saudi Arabia na baraza la mpito la kusini mwa Yemen.