Russia na Hizbullaha ya Lebanon zafikia makubaliano ya kuimarisha ushirikiano
Afisa wa Mahusiano ya Kigeni wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, harakati hiyo imefikia makubaliano na Russia ya kuimarisha ushirikiano baina yao kuhusiana na masuala yote yanayohuusu maslahi ya pamoja.
Ammar Musawi amesema hayo katika mahojiano yake na Kanali ya Televisheni ya al-Alam na kubainisha kwamba, Russia na Hizbullah zina mitazamo ya pamoja kuhusiana na masuala muhimu ya kieneo na kimataifa.
Afisa wa Mahusiano ya Kigeni wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ameeleza kwamba, Moscow inafahamu na kudikiri misimamo ya harakati hiyo na inaiunga mkono.
Aidha amesema, kukombolewa kikamilifu ardhi ya Syria na kukarabatiwa nchi hiyo pamoja na kurejea wakimbizi wa Kisyria ni baadhi ya zilizokuwa ajenda kuu za mazungumzo ya Hizbullah na Russia huko Moscow,
putin
Russia kwa upande wake ambapo ujumbe wake katika mazungumzo hayo na Hizbullah mjini Moscow uliongozwa na Sergey Lavrov, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hiyo imesisitiiza kuwa, inafanya kadiri inavyoweza kusaidia juhudi za kuupatia ufumbuzi mgogoro wa kuundwa serikali nchini Lebanon.
Hivi karibuni Sergey Lavrov, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia alisisitiza pia kuwa, ni lazima mamlaka ya kujitawala Syria yaheshimiwe. Aidha alisema, kurejea Syria katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ni jambo lisilo la shaka na kwamba, hatua hiyo ni kwa maslahi ya amani na uthabiti wa eneo lote la Asia Magharibi.