Jeshi la Yemen lakomboa eneo muhimu magharibi mwa Ma'rib
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i68014-jeshi_la_yemen_lakomboa_eneo_muhimu_magharibi_mwa_ma'rib
Duru za kijeshi za Yemen zimetangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo kwa kushirikiana na kamati za kujitolea za wananchi limekomboa aneo muhimu la al Atif, magharibi mwa mkoa wa Ma'rib.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 18, 2021 03:28 UTC
  • Jeshi la Yemen lakomboa eneo muhimu magharibi mwa Ma'rib

Duru za kijeshi za Yemen zimetangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo kwa kushirikiana na kamati za kujitolea za wananchi limekomboa aneo muhimu la al Atif, magharibi mwa mkoa wa Ma'rib.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, jeshi la Yemen na vikosi vya kujitolea vya wananchi wameendelea kusonga mbele katika ukombozi wa mkoa wenye utajiri wa mafuta la Ma'rib, mashariki mwa nchi hiyo kwa kukomboa eneo jingine muhimu la al Atif.

Mtando wa Ma'rib Press umeripoti kuwa, usiku wa kuamkia leo, jeshi na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa Yemen vimefanikiwa kulikomboa kikamilifu eneo hilo lililoko magharibi mwa Ma'rib na kwamba mapigano hivi sasa yanaendelea katika wilaya muhumi ya Sarawih.

Baada ya kufanikiwa kukomboa milima ya kiistratijia ya eneo la al Atif, wanamapambano wa Yemen waliendesha mapambano makali na magaidi wa al Qaida na askari wa madola vamizi yanayoongozwa na Saudi Arabia, kabla ya kulidhibiti kikamilifu eneo hilo usiku wa kuamkia leo baada ya kuwaangamiza na kuwafurusha askari vamizi na magaidi wao katika eneo hilo.