Yemen yashambulia vituo 'hasasi' vya kijeshi vya Saudia jijini Riyadh
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i68550-yemen_yashambulia_vituo_'hasasi'_vya_kijeshi_vya_saudia_jijini_riyadh
Msemaji wa vikosi vya jeshi la Yemen ametangaza habari ya kushambuliwa vituo nyeti na hasasi vya Saudi Arabia katika mji mkuu Riyadh.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 01, 2021 06:40 UTC
  • Yemen yashambulia vituo 'hasasi' vya kijeshi vya Saudia jijini Riyadh

Msemaji wa vikosi vya jeshi la Yemen ametangaza habari ya kushambuliwa vituo nyeti na hasasi vya Saudi Arabia katika mji mkuu Riyadh.

Brigedia Jenerali Yahya Saree amesema hayo leo katika ujumbe aliotuma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na kuongeza kuwa: Vikosi vya Yemen vimefanikiwa kuvilenga vituo muhimu vya Saudia jijini Riyadh kwa kutumia ndege nne zisizo na rubani (droni).

Amesema droni hizo za vikosi vya Yemen vimelenga kwa usahihi mkubwa vituo vilivyokusudiwa ndani ya mji mkuu wa Saudia, katika shambulio halali la ulipizaji kisasi.

 Ameongeza kuwa, jeshi na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa Yemen vitaacha kuipiga kwa makombora Saudia iwapo tu wavamizi hao wataacha kuizingira na kuishambulia nchi yao.

Brig. Jen. Yahya Saree

Machi 2015, Saudi Arabia kwa msaada wa Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel, Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) na baadhi ya nchi za Ulaya na Kiarabu kama Uingereza na Sudan, ilianzisha mashambulizi ya kivamizi ya pande zote dhidi ya taifa maskini la Kiarabu na Kiislamu la Yemen.

Wavamizi hao walikuwa na ndoto ya kuvimaliza vita hivyo katika kipindi cha wiki chache tu. Hata hivyo huu ni mwaka wa 7 na kadiri siku zinavyopita, ndivyo wananchi wa Yemen wanavyozidi kuwa imara katika muqawama na kujihami kwao kishujaa.