Ansarullah Yemen: Madai ya Marekani kuhusu kuisaidia Yemen ni masikhara
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i68564-ansarullah_yemen_madai_ya_marekani_kuhusu_kuisaidia_yemen_ni_masikhara
Msemaji wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameyataja madai ya Marekani na waitifaki wake kuhusu kuisaidia Yemen kuwa ni istihzai na masikhara na kueleza kuwa, kama ingeweza Marekani ingewanyima hata hewa wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Apr 01, 2021 22:23 UTC
  • Ansarullah Yemen: Madai ya Marekani kuhusu kuisaidia Yemen ni masikhara

Msemaji wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameyataja madai ya Marekani na waitifaki wake kuhusu kuisaidia Yemen kuwa ni istihzai na masikhara na kueleza kuwa, kama ingeweza Marekani ingewanyima hata hewa wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu.

Muhammad Abdulsalam, Mkuu wa Timu ya Mazungumzo ya Yemen na msemaji wa harakati ya Ansarullah ya nchi hiyo amewaambia wavamizi wa Yemen kuwa, mnaanzisha vita dhidi ya nchi yangu, mnaizingira kwa pande zote na kuwanyima kila kitu wananchi wa Yemen; na kisha mnafanya masikhara kwamba mnaisaidia Yemen. 

Muhammad Abdulsalam amesisitiza kwamba, Yemen inapasa kuachwa yenyewe itekeleze na kusimamia masuala yake kwa izza na  heshima, na wala haihitaji masuala ya kipumbavu kama hayo.  

Maafa ya vita vya muungano vamizi wa Saudia na washirika wake dhidi ya wananchi wa Yemen

Saudi Arabia huku ikiungwa mkono kwa hali na mali na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati), Marekani, utawala wa Kizayuni, Uingereza na nchi kadhaa nyingine mwezi kama vile Sudan, mwezi Machi mwaka 2015 ilianzisha mashambulizi ya kijeshi ya pande zote dhidi ya Yemen na kuiwekea mzingiro wa angani, baharini na nchi kavu nchi hiyo maskini ya Kiarabu. 

Hadi sasa Wayemeni zaidi ya elfu 16 wameshauawa katika vita hivyo vya muungano vamizi unaoongozwa na Saudia, huku makumi ya maelfu ya  wakijeruhiwa na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi.