Umoja wa Mataifa: Mgogoro wa wakimbizi ni wa dunia nzima
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i7219-umoja_wa_mataifa_mgogoro_wa_wakimbizi_ni_wa_dunia_nzima
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya wakimbizi amesema kuwa, mgogoro wa wakimbizi ni tatizo la dunia nzima.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 16, 2016 23:50 UTC
  • Umoja wa Mataifa: Mgogoro wa wakimbizi ni wa dunia nzima

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya wakimbizi amesema kuwa, mgogoro wa wakimbizi ni tatizo la dunia nzima.

Televisheni ya Press TV imemnukuu Filippo Grandi akisema hayo jana (Jumatatu) na kuongeza kuwa, hivi sasa kuna wakimbizi milioni 60 kote ulimwenguni na kwamba suala la kuwasaidia wakimbizi hao ni la dunia nzima.

Grandi ameongteza kuwa, wakimbizi wa Syria wamefika hadi mashariki mwa Asia na Caribbean na hili linazidi kuthibitisha kuwa mgogoro wa wakimbizi unataka ushirikiano wa dunia nzima kuutatua.

Amesema, suala la kuwasaidia wakimbizi linabidi lipewe kipaumbele zaidi vinginevyo Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa litashindwa kutekeleza vizuri majukumu yake.

Aidha amekiri kuwa mazungumzo ndiyo njia bora ya kutatua mgogoro wa wakimbizi na kuongeza kuwa, kufunga mipaka na kuzuia kuingia wakimbizi katika baadhi ya nchi hakuwezi kutatua mgogoro huo.