Qatar yatoa msaada kwa Yemen kusaidia ili upatikanaji wa chakula
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i72664-qatar_yatoa_msaada_kwa_yemen_kusaidia_ili_upatikanaji_wa_chakula
Amir wa Qatar ameagiza kutolewa dola milioni mia moja ili kusaidia usalama wa chakula huko Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 22, 2021 22:02 UTC
  • Qatar yatoa msaada kwa Yemen kusaidia ili  upatikanaji wa chakula

Amir wa Qatar ameagiza kutolewa dola milioni mia moja ili kusaidia usalama wa chakula huko Yemen.

Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Aal Thani ameagiza kutolewa dola milioni mia moja kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Mpango wa Chakula Duniani (WFP) huko Yemen katika kuhakikisha kwamba usalama wa chakula unakuweko huko Yemen na kuzuia ukosefu wa chakula. 

Kabla ya hapo, Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ulitahadharisha kuhusu uwezedkano wa kutokea janga kubwa la ukosefu wa chakula nchini Yemen na kusema kuwa Wayemeni milioni 16 wanakabiliwa na njaa. 

Mark Lowcock Afisa wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa pia ameeleza kuwa, karibu asilimia 80 ya wananchi wa Yemen wanahitaji misaada ya chakula, na watoto laki tano walio na umri wa chini ya miaka mitano wana utapiamlo mkali.

Lowcok amezitolea mwito nchi za pambizoni mwa eneo la Ghuba ya Uajemi kutoa misaada kwa ajili ya watu wa Yemen ili kuzuia baa la njaa na la kibinadamu. 

Mark Lowcock

Wakati huo huo, gazeti la Economist pia limeandika: Yemen inashika nafasi 113 katika vigezo vya usalama wa chakula duniani na imekuwa na hali mbaya zaidi katika uwanja huo mwaka 2020.