Spika Nabih Berri: Silaha za muqawama zina udharura kwa Lebanon
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i79968-spika_nabih_berri_silaha_za_muqawama_zina_udharura_kwa_lebanon
Spika wa Bunge la Lebanon amesema, muqawama na silaha za muqwama ni hitajio la kitaifa kwa ajili ya kuzuia uchu na tamaa ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2026-08-08T07:03:00+00:00 )
Feb 04, 2022 04:40 UTC
  • Spika Nabih Berri: Silaha za muqawama zina udharura kwa Lebanon

Spika wa Bunge la Lebanon amesema, muqawama na silaha za muqwama ni hitajio la kitaifa kwa ajili ya kuzuia uchu na tamaa ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Nabih Berri ameeleza kuwa, kuwepo kwa silaha za muqawama ni matokeo ya uvamizi na ukaliaji ardhi kwa mabavu wa utawala wa Kizayuni; na madamu kuna japo dhiraa moja tu ya ardhi ya Lebanon inayokaliwa kwa mabavu na Israel, nchi hiyo itaendelea kuuhitaji muqawama.

Aidha, Spika wa Bunge la Lebanon amesema, anakaribisha hatua yoyote ya kuzikurubisha pamoja nchi za Kiarabu na akaongeza kwamba, hilo halitayumkinika bila Syria kurejea kwenye Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na kurudi Waarabu kwa Syria.

Kuhusiana na uchaguzi wa bunge la Lebanon, Nabih Berri amesema, hataruhusu kufanyika kwa uchaguzi huo kucheleweshwe hata kwa dakika moja.

Bunge la Lebanon limetangaza kuwa uchaguzi wa wabunge utafanyika tarehe 27 ya mwezi ujao wa Machi.../