Mamluki 500 wa muungano vamizi wauawa na kujeruhiwa kaskazini mwa Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i81384-mamluki_500_wa_muungano_vamizi_wauawa_na_kujeruhiwa_kaskazini_mwa_yemen
Zaidi ya mamluki 500 raia wa Saudia na Sudan wameangamizwa na kujeruhiwa katika opereseheni ya jeshi na kamati za ukombozi za wananchi wa Yemen katika mkoa wa Hajjah, wa kaskazini mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 14, 2022 23:08 UTC
  • Mamluki 500 wa muungano vamizi wauawa na kujeruhiwa kaskazini mwa Yemen

Zaidi ya mamluki 500 raia wa Saudia na Sudan wameangamizwa na kujeruhiwa katika opereseheni ya jeshi na kamati za ukombozi za wananchi wa Yemen katika mkoa wa Hajjah, wa kaskazini mwa nchi hiyo.

Sasa hivi vita vya Yemen vimeingia kwenye hatua nyeti mno. Baada ya kupita zaidi ya miaka saba tangu Saudi Arabia ilipounda muungano vamizi na kuivamia nchi hiyo maskini ya Kiarabu, jeshi la Yemen na kamati za ukomvozi za kujitolea za wananchi wa nchi hiyo limekuwa likipata ushindi mkubwa katika medani tofauti yakiwemo maeneo ya katikati na magharibi mwa Yemen.

Shirika la habari la FARS limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, vikosi vya jeshi la Yemen kwa kushirikiana na kamati za ukombozi za kujitolea za wananchi wa nchi hiyio limefanya mashambulio makubwa katika maficho ya mamluki hao ambao ni raia wa Saudia na Sudan magharibi mkoa wa Hajjah wa kaskazini maghribi wa Yemen na kuangamiza mamia ya mamluki hao vamizi.

Baadhi ya wanajeshi vamizi wa Sudan walioangamizwa nchini Yemen

 

Operesheni hiyo ya siku mbili imefanikiwa pia kukomboa makumi ya maeneo ikiwemo miji na vijiji vya mkoa huo kutoka kwenye makucha ya wavamizi wa nchi hiyo.

Tangu mwezi Machi 2015, Saudi Arabia kwa kushirikiana na nchi kama Umoja wa Falme za Kiarabu na kwa silaha na baraka kamili ya madola ya Magharibi hasa Marekani, ilianzisha mashambulizi ya pande zote dhidi ya nchi ya Waislamu ya Yemen. Hata hivyo wavamizi hao wameshindwa kufikia malengo yao waliyotangaza mwanzoni mwa uvamizi wao yaani kumrejesha madarakani rais wa zamani wa Yemen aliyejiuzulu na kutoroka nchi, Abdu Rabbuh Mansour Hadi; kutokana na muqawama na mapambano ya kishujaa ya wananchi wa Yemen.