Hamas: Mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni yanaendelea hadi mwisho
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i84218-hamas_mapambano_dhidi_ya_utawala_wa_kizayuni_yanaendelea_hadi_mwisho
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel yataendelea hadi wavamizi hao wa ardhi za Palestina na za Waislamu watakapotimuliwa kikamilifu katika ardhi hizo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 31, 2022 03:04 UTC
  • Hamas: Mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni yanaendelea hadi mwisho

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel yataendelea hadi wavamizi hao wa ardhi za Palestina na za Waislamu watakapotimuliwa kikamilifu katika ardhi hizo.

Kituo cha Upashaji Habari ya Palestina kimemnukuu Fauzi Barhoum akisema hayo jana na kuongeza kuwa, kuna pande nyingi hivi sasa zinajaribu kuwasiliana na HAMAS ili kujaribu kupunguza wasiwasi na moto wa kuingia kwenye vita vikubwa na utawala wa Kizayuni baada ya Wazayuni hao kukaidi miito yote ya kuwataka wasifanye "Maandamano ya Bendera" lakini msimamo wa HAMAS ni kuwa vita na utawala huo pandikizi vitaendelea hadi utakapotimuliwa kikamilifu katika ardhi za Palestina.

Msemaji huyo wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina vile vile amesisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni wenyewe ndilo tatizo. Utawala huo unataka kuidhibiti Quds na Msikiti wa al Aqsa. Amesema, maonyo yaliyotolewa na muqawama wa Palestina yamewatia woga Wazayuni na yamezuia kufanyika "Maandamano ya Bendera" katika sehemu nyingi.

Fauzi Barhoum

 

Vile vile amesema, makundi ya mapambano ya Kiislamu ya Palestina yamewaonesha wanajeshi wa Israel nguvu zao kutokana na wananchi wa Palestina kujitokeza kwa wingi na muda wote kupambana na uvamizi wa mara kwa mara wa Wazayuni katika Msikiti wa al Aqsa. Amesema: Sasa hivi muqawama umeingia kwenye vita vinne na Wazayuni ambavyo ni  vita vya taarifa za kijasusi, vita vya kijeshi, vita vya wananchi na vita vya kidiplomasia.

Msemaji huyo wa HAMAS vile vile amelitaka taifa la Palestina kuwa na mkakati wa kitaifa, Kiislamu na Kiarabu katika daraja zote ili kuufanya utawala wa Kizayuni wa Israel ukome kuvunjia heshima matukufu ya Wapalestina na Waislamu. Amesema utawala wa Kizayuni ni thishio kwa nch zote za Kiislamu na Kiarabu.