Wapalestina 62 wameshauawa shahidi tangu mwanzoni mwa mwaka 2022
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i84316-wapalestina_62_wameshauawa_shahidi_tangu_mwanzoni_mwa_mwaka_2022
Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa, Wapalestina 62 washauliwa shahidi na wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2022.
(last modified 2026-07-02T04:13:23+00:00 )
Jun 02, 2022 22:41 UTC
  • Wapalestina 62 wameshauawa shahidi tangu mwanzoni mwa mwaka 2022

Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa, Wapalestina 62 washauliwa shahidi na wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2022.

Kwa mujibu wa al Quds al Arabi, Wizara ya Afya ya Palestina imetoa ripoti maalumu na kufafanua kwamba, Wapalestina hao wameuliwa shahidi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, Quds Mashariki na Ukanda wa Ghaza. Mauaji ya karibuni zaidi ni ya kijana wa miaka 29 wa Kipalestina ambaye aliuliwa shahidi asubuhi ya jana Alkhamisi wakati wanajeshi Wazayuni walipovamia kambi ya wakimbizi ya al Dheisheh ya Wapalestina, kusini mwa Bayt al Laham.

Kila leo Wazayuni wanavamia maeneo tofauti ya Wapalestina na kuwateka nyara, kuwajeruhi na kuwaua shahidi Wapalestina wasio na ulinzi, kwa sabaha ya kufanikisha malengo ya kujitanua ya Israel.

Baadhi ya vijana wa Kipalestina waliouliwa shahidi na wanajeshi makatili wa Israel

 

Usiku wa kuamkia jana Alkhamisi pia, kijana mwingine wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 24 aliuliwa shahidi katika kitongoji cha Ya'bad huko Jenin. Kabla ya hapo pia, wanajeshi Wazayuni walimpiga risasi na kumuua kijana mwingine wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 31 katika lango la kuingilia kambi ya wakimibizi ya al Urub huko kaskazini mwa al Khalil.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mohammad Ibrahim Shtayyeh amesema kuwa utawala wa Kizayuni unafanya mauaji ya makusudi dhidi ya Wapalestina ili kuishikilia isianguke serikali tete ya Kizayuni inayoongozwa na waziri mkuu, Naftali Bennett.