Israel yatiwa kiwewe na msimamo wa UN kuwatetea Wapalestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i907-israel_yatiwa_kiwewe_na_msimamo_wa_un_kuwatetea_wapalestina
Utawala wa kizayuni wa Israel umetiwa kiwewe na matamshi yaliyotolewa hivi karibuni ya Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ya kuwatetea Wapalestina ambao ardhi zao zinakaliwa kwa mabavu na Wazayuni maghasibu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 09, 2016 14:54 UTC
  • Israel yatiwa kiwewe na msimamo wa UN kuwatetea Wapalestina

Utawala wa kizayuni wa Israel umetiwa kiwewe na matamshi yaliyotolewa hivi karibuni ya Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ya kuwatetea Wapalestina ambao ardhi zao zinakaliwa kwa mabavu na Wazayuni maghasibu.

Danny Danon, Balozi wa utawala huo haramu katika Umoja wa Mataifa amemwandikia barua Ban Ki-moon akimtuhumu kuwa, eti anaunga mkono 'ugaidi' kutokana na kauli yake aliyotoa mwezi uliopita mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Katika mkutano huo wa Baraza la Usalama, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema harakati za kulinda ardhi zinazofanywa na Wapalestina ni jibu ambalo yeyote angelitarajia kutoka kwa watu au kaumu ambayo ardhi yao imeghusubiwa. Ban Ki-moon aliitaka Israe kusimamisha ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi inazozikalia kwa mabavu akisisitiza kuwa, ujenzi huo sio chokochoko tu kwa Wapestina bali kwa jamii ya kimataifa kwa ujumla.

Licha ya barua hiyo ya balozi wa utawala haramu wa Israel katika Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, Msemaji wa Ban Ki-moon amesisitiza kuwa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atasimama na kila neno alilolitamka kuhusu kughusubiwa ardhi ya Wapalestina.