Wapalestina wapinga mkutano na Israel ulioandaliwa na US huko Jordan
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i94494-wapalestina_wapinga_mkutano_na_israel_ulioandaliwa_na_us_huko_jordan
Maelfu ya Wapalestina wamefanya maandamano katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kulalamikia mkutano eti wa kiusalama ulioandaliwa na Marekani huko Jordan, siku chache baada ya jeshi katili la Israel kufanya mashambulizi ya umwagaji damu huko Jenin.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 26, 2023 23:01 UTC
  • Wapalestina wapinga mkutano na Israel ulioandaliwa na US huko Jordan

Maelfu ya Wapalestina wamefanya maandamano katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kulalamikia mkutano eti wa kiusalama ulioandaliwa na Marekani huko Jordan, siku chache baada ya jeshi katili la Israel kufanya mashambulizi ya umwagaji damu huko Jenin.

Wapalestina walijitokeza kwa wingi kwenye maandamano hayo yaliyofanyika mapema Jumapili katika barabara zinazoizunguka kambi ya wakimbizi ya Dheisheh, kusini mwa Beitu Lahm (Bethlehem), kabla ya kuanza mkutano huo wa Jordan baadaye hiyo jana.

Waandamanaji hao wamekosoa mkutano huo wa maafisa wa ngazi za juu wa utawala haramu wa Israel, Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Marekani, Misri na Jordan katika mji wa kitalii wa Aqaba.

Maandamano kama hayo yameshuhudiwa pia katika mji wa Jenin, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi, ambapo waandamanaji wa Kipalestina wamepiga nara za kulaani mkutano huo.

Wawakilishi wa makundi ya muqawama walioshiriki kwenye maandamano hayo wamewakosoa vikali wajumbe wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kwa kwenda kushiriki mkutano huo ulioandaliwa na Marekani, wakisisitiza kuwa kikao hicho hakitakuwa na tija.

Mahmoud Abbas (kulia) na Benjamin Netanyahu

Taarifa ya pamoja na makundi ya muqawama imesema: Taasisi za Mamlaka ya Ndani ya Palestina badala ya kushiriki mikutano ya kiusalama ya namna hiyo inayoandaliwa na Ikulu ya White House ya Marekani, zinapasa kufanya jitihada za kuimarisha umoja wa kitaifa na kambi ya muqawama.

Basem Naim, Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa ya Harakati ya Mapambanoya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema lengo la mkutano huo wa Aqaba ni kupanda mbegu za chuki na kuibua mifarakano miongoni mwa Wapalestina, ili kwa utaratibu huo waweze kubinya mrengo wa muqawama.