Rais wa Israel ataka kusitikishwa haraka mageuzi ya mahakama ya Netanyahu
Rais Isaac Herzog wa Israel amemtaka Waziri Mkuu wa utawala huo wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu kuachana na mpango wake wa kile kinachoitwa 'mageuzi wa mahakama'.
Kadhalika Rais Herzog amemtaka Netanyahu ampige kalamu nyekundu Waziri wa masuala ya vita wa utawala huo ghasibu, Yoav Gallant kutokana na misimamo yake mikali, huku duru za habarin zikidokeza kuwa Netanyahu ameanza kulegeza kamba juu ya kadhia hiyo kufuatia mashinikizo na maandamano ya Waisraeli.
Katika ujumbe wa Twitter, Herzog amesema: Tumeshuhudia taswira za kuogofya usiku huu (wa jana Jumapili). Namuomba Waziri Mkuu, pamoja na maafisa wa serikali na muungano wake wafahamu kuwa taifa zina linakabiliwa na taharuki. Usalama, uchumi na jamii, vyote vinabailiwa na tishio la hatari.
Ameendelea kusema kuwa, "Kwa ajili ya umoja wa watu wa Israel, kwa ajili ya uwajibikaji, nakuomba usitishe mara utekelezaji wa mageuzi ya mahakama. Huu si wakati wa siasa, huu ni wakati wa kuonyesha uongozi na uwajibikaji."
Wakati huohuo, duru za habari zinaarifu kuwa Netanyahu amefanya mazungumzo na maafisa wake kuhusuu uwezekano wa kufutilia mbali mageuzi hayo, kufuati wimbi la maandamano la wiki kadhaa.
Maelfu ya walowezi wa Kizayuni wameandamana kwa wiki 11 mfululizo kupinga mpango huo wa mageuzi ya mahakama unaoshinikizwa na Netanyahu.
Duru za habari zinaarifu kuwa, kutokana na mashinikizo hayo,Yoav Gallant, Waziri wa Vita wa Israel anatazamiwa kutangaza kusimamishwa kwa mpango huo wa kuifanyika mageuzi idara ya mahakama ya utawala huo bandia wakati wowote kuanzia sasa.