-
Yemen yawaonya Waisrael: Rudini mlikotoka kwenye nchi zenu za asili; hatutaiacha Ghaza peke yake
Jan 06, 2025 03:39Mwanachama mwandamizi wa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen amewashauri walowezi haramu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu waondoke katika maeneo hayo kurejea walikotoka kwa sababu Yemen haitasitisha oparesheni zake za kulipiza kisasi dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Reuters ladai HAMAS imeafiki kuwaachia huru mateka 34 wa utawala wa Kizayuni
Jan 06, 2025 03:09Shirika la habari la Reuters limedai kuwa, Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imekubali kuwaachia huru mateka 34 wa Kizayuni ambao orodha yao imetolewa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Waziri Mkuu wa Iraq: Jenerali Soleimani alikuwa bega kwa bega na Iraq katika nyakati ngumu kabisa
Jan 06, 2025 02:50Waziri Mkuu wa Iraq amemsifu na kumuenzi kamanda mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kupambana na ugaidi Luteni Jenerali Shahidi Qassem Soleimani, akisema, kamanda huyo alisimama bega kwa bega na nchi hiyo ya Kiarabu katika nyakati ngumu na za changamoto kubwa zaidi.
-
Makundi yanayopigana kwa niaba ya US na Uturuki nchini Syria yatwangana, zaidi ya 100 wauawa
Jan 05, 2025 23:36Wanamgambo zaidi ya 100 wameuawa katika muda wa siku mbili zilizopita kaskazini mwa Syria katika mapigano kati ya makundi yanayoungwa mkono na Uturuki na vikosi vya Wakurdi vinavyoungwa mkono na Marekani. Hayo ni kwa mujibu wa kundi linalofuatilia habari za vita lenye makao yake London, Uingereza.
-
Katika mwaka mmoja tu wa 2024, Israel ilibomoa kikamilifu Misikiti 815 na kuharibu 151 Ghaza
Jan 05, 2025 23:36Katika mwaka uliomalizika wa 2024, wanajeshi wa utawala wa Kiziayuni wa Israel walibomoa kikamilifu Misikiti 815 na kuharibu mingine 151 katika Ukanda wa Ghaza. Hayo yameelezwa katika ripoti iliyotolewa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Dini ya Palestina.
-
Wanajeshi magaidi wa Israel watimka Ghaza baada ya kuangamizwa 13 kati yao
Jan 05, 2025 23:35Duru za utawala wa Kizayuni zimetangaza kuwa, wanajeshi wa Israel wamekimbia kaskazini mwa Ghaza baada ya kupata kipigo kikali kutoka kwa wanamapambano wa Palestina hasa baada ya kuangamizwa wanajeshi 13 wa Israel kwenye eneo hilo.
-
Kuendelea misaada ya silaha ya Marekani kwa Israel
Jan 05, 2025 23:32Jinai za Israel dhidi ya Wapalestina wanaoishi Gaza zinaendelea kwa kuungwa mkono wa nchi za Magharibi hususan Marekani.
-
Kwa siku 3 Israel yashambulia zaidi ya mara 100 Ghaza, yaua Wapalestina zaidi ya 200, wengi wao ni wanawake na watoto
Jan 05, 2025 11:06Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewaua Wapalestina wasiopungua 88 katika muda wa siku moja katika maeneo kadhaa ya Ukanda wa Ghaza.
-
Kukosolewa mauaji ya umati ya Israel katika Ukanda wa Gaza
Jan 05, 2025 09:01Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichoitishwa kwa ajili ya kuchunguza hali ya Gaza kilifanyika kwa mara nyingine tena. Ukitoa Marekani, washiriki wengine wa mkutano huo wamekosoa "mauaji ya kimbari" ya Wazayuni dhidi ya watu wa Gaza.
-
Kwa mara nyingine, Israel yashindwa kutungua kombora la Yemen
Jan 05, 2025 07:58Mapema leo Jumapili, harakati ya Ansarullah ya Yemen imetangaza kuwa, kombora lililorushwa kutoka nchini humo limepiga kiustadi mkubwa shabaha iliyokusudiwa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni na kwamba madai ya Israel ya kutungua kombora hilo hayana ukweli wowote.