-
Wapalestina 37 wauawa shahidi katika mashambulio ya Israel huko Gaza
Apr 28, 2024 03:50Wapalestina 37 wameuawa shahidi katika mashambulio ya anga ya utawala wa Kizayuni wa Israel katikati na kusini mwa Ukanda wa Gaza.
-
Amnesty International: Ubaguzi wa apartheid wa Israel dhidi ya Wapalestina hauwezi kukanushwa
Apr 28, 2024 00:57Katibu Mkuu wa Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International amesema kuwa, utawala wa Israel umetekeleza ubaguzi wa apartheid dhidi ya Wapalestina. Agnes Callamard amesema kuwa, ameshangazwa mno na utumiaji mabavu wa kimfumo wa utawala ghasibu wa Israel.
-
UN yaunga mkono maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu Marekani ya kuwatetea watu wa Gaza
Apr 28, 2024 00:56Stephen Dujaric Msemaji wa Umoja wa Mataifa jana Ijumaa alisema katika radiamali yake kwa maandamano yanayoendelea kufanywa na wanafunzi wa vyuo vikuu huko Marekani katika kuwaunga mkono watu wa Gaza na kupinga mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa eneo hilo kwamba: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni mfuasi na mungaji mkono mkubwa wa uhuru wa kujieleza, ikiwa ni pamoja na huko Marekani; na anaunga mkono haki ya wananchi ya kufanya maandamano kwa amani.
-
Yemen yashambulia Meli za Uingereza katika Bahari Nyekundu
Apr 27, 2024 04:50Shirika la Operesheni za Baharini la Uingereza (UKMTO) lilitangaza jana Ijumaa, kwamba meli yake karibu na pwani ya Yemen imelengwa na kuharibiwa kwa takribani makombora mawili.
-
Kufuatia jinai za Israel, Gaza inahitaji miaka 14 kutegua mabomu na kuwa salama
Apr 27, 2024 04:34Kwa muda wa karibu miezi saba sasa, utawala katili wa Israel umekuwa ukidondosha mabomu kila siku katika Ukanda wa Gaza na sasa Umoja wa Mataifa unasema zoezi la kutegua mabomu ambayo hayajalipuka eneo hilo linaweza kuchukua muda miaka 14.
-
Mbali na walionyofolewa viungo, Wapalestina wengine walizikwa wakiwa hai kwenye makaburi ya halaiki Ghaza
Apr 26, 2024 23:17Wahudumu wa afya, timu za uokoaji na mashirika ya kutetea haki za binadamu yanawashutumu askari vamizi wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuwanyofoa viungo Wapalestina na hata kuwazika baadhi yao wakiwa hai kwenye makaburi ya halaiki yaliyogunguliwa kwenye eneo la karibu na Hospitali ya Nasser huko Ukanda wa Ghaza, baada ya askari hao katili kuondoka katika eneo hilo Aprili 7 kufuatia mashambulizi ya ardhini ya miezi minne.
-
Hamas: Miili ya makaburi ya umati Gaza ifanyiwe uchunguzi
Apr 26, 2024 23:17Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetoa wito wa kutumwa timu za uchunguzi ili kutambua miili iliyogunduliwa kwenye makaburi ya halaiki katika Ukanda wa Gaza.
-
Vikosi vya Yemen vyashambulia meli ya Israel, Bandari ya Eilat kuonyesha mshikamano na Gaza
Apr 26, 2024 04:11Vikosi vya Wanajeshi wa Yemen vimefanikiwa kulenga meli ya utawala wa Israel katika Ghuba ya Aden pamoja na Bandari ya Eilat katika sehemu ya kusini ya maeneo yanayokaliwa kwa mabavu (Israel) katika operesheni mpya zinazoiunga mkono Palestina.
-
Amir-Abdollahian: White House inapasa kusitisha haraka uungaji mkono wake kwa jinai za kivita za Israel
Apr 25, 2024 23:39Akikosoa ukandamizaji na unyanyasaji wa askari usalama vya Marekani dhidi ya wahadhiri na wanafunzi wanaopinga jinai za kivita za utawala ghasibu wa Israel, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: Ikulu ya Marekani inapasa kusitisha haraka iwezekanavyo uungaji mkono wake kwa jinai za kivita za utawala ghasibu wa Israel.
-
UN: Hatuwezi kuwaambia Wapalestina wasubiri misaada
Apr 25, 2024 23:36Jumuiya ya kimataifa ina jukumu na wajibu wa kufanya kazi kufanikisha kukwamua Gaza lakini hatuwezi kuwaambia raia Wapalestina wanaoteseka wasubiri, amesema afisa wa Umoja wa Mataifa anayehusika na ufikishaji wa misaada kwenye eneo hilo linalokabiliwa na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala haramu wa Israel.