-
Kuwait yachukizwa na hatua ya balozi wa Marekani kutetea maingiliano ya kimwili ya watu wa jinsia moja
Jun 03, 2022 23:43Wizara ya Mambo ya Nje ya Kuwait imemwita balozi mdogo wa Marekani nchini humo kufuatia hatua ya ubalozi wao kutoa matamshi ya kutetea na kuunga mkono maingiliano ya kimwili ya watu wa jinsia moja.
-
Wazayuni wakivamia tena Kibla cha Kwanza cha Waislamu, jamii ya kimataifa kimya!
Jun 03, 2022 06:12Licha ya kwamba taasisi mbalimbali za kimataifa zimetoa tangazo rasmi la kusisitiza kuwa Wazayuni hawahusiki kivyovyote vile na maeneo matakatifu ya Wapalestina ukiwemo Msikiti wa al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu, lakini kila leo Wazayuni hao wanauvamia Msikiti huo na jamii ya kimataifa imekaa kimya ikiangalia kwa macho tu.
-
Wapalestina 62 wameshauawa shahidi tangu mwanzoni mwa mwaka 2022
Jun 02, 2022 22:41Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa, Wapalestina 62 washauliwa shahidi na wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2022.
-
Yaliyojiri katika kikao cha kwanza cha Bunge la Lebanon
Jun 02, 2022 22:11Kikao cha kwanza cha bunge la Lebanon kimefanyika kwa kuchaguliwa Spika na Naibu Spika wa bunge hilo.
-
Bunge la Israel lapasisha uamuzi wa kujinaisha upeperushaji wa bendera ya Palestina
Jun 02, 2022 05:41Bunge la utawala haramu wa Israel limepasisha uamuzi wa awali wa kupiga marufuku kutundikwa na kupeperushwa bendera ya Palestiina katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel.
-
Makubaliano ya serikali ya Islamabad na Taliban ya Pakistan ya kusimamisha vita kikamilifu
Jun 01, 2022 21:54Taarifa kutoka Afghanistan zinasema kuwa, kumepigwa hatua nzuri katika mazungumzo baina ya serikali ya Islamabad na kundi la Taliban la Pakistan linalojulikana kwa jina la Tehrik-i-Taliban Pakistan (TTP) kwa upatanishi wa kundi la Taliban la Afghanistan. Taarifa hizo zinasema kuwa pande mbili zimefikia makubaliano ya kusimamisha vita kikamilifu baina yao katika mazungumzo yanayoendelea mjini Kabul.
-
Rais Mahmoud Abbas alaani kimya cha jamii ya kimataifa kwa jinai za Israel
Jun 01, 2022 21:53Mamlaka ya Ndani ya Palestina imelaani vikali kimya cha jamii ya kimataifa na kutochukua kwake hatua yoyote ya maana kukabiliana na vitendo vya kinyama na jiinai za utawala ghasaibu wa Israel huko Palestina.
-
Wanajeshi wa Israel wampiga risasi na kumuua mwanamke Mpalestina
Jun 01, 2022 05:45Wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wamempiga risasi na kumuua shahidi mwanamke Mpalestina kwa kisingizio kuwa eti alikuwa analenga kutekeleza shambulizi la kujitolea kufa shahidi.
-
Palestina: Si msikiti wa Al Aqsa pekee Palestina unaovamiwa na kuvunjiwa heshima na Wazayuni
Jun 01, 2022 03:37Wizara ya Waqfu ya Palestina imetangaza kuwa, mbali na Al Aqsa, kuna misikiti mingine mingi Palestina katika Ufukwe wa Magharibi inayovamiwa na kuvunjiwa heshima na wazayuni.
-
Askari wanne wa Kizayuni, Wapalestina watatu wajeruhiwa katika mapigano yaliyotokea Msikiti wa Al Aqsa
May 31, 2022 22:25Askari wanne wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na Wapalestina watatu wamejeruhiwa katika mapigano yaliyotokea Jumanne kati ya jeshi la Kizayuni na Wapalestina katika msikiti wa al Aqsa.