Oct 22, 2023 03:20 UTC
  • Balozi wa Korea Kaskazini nchini Russia: Marekani itashindwa huko Ukraine kama ilivyofeli Afghanistan

Balozi wa Korea Kaskazini nchini Russia amelaani uungaji mkono na misaada ya kijeshi ya Marekani kwa Ukraine na kusema, mara hii pia Marekani itashindwa na kufeli kama ilivyokuwa huko Afghanistan.

Sin Hong Chol, balozi wa Korea Kaskazini nchini Russia amesisitiza  kwamba, gharama kubwa zinazotumiwa na Marekani nchini Ukraine ni kinyume na maslahi ya nchi za Ulaya, kwa sababu Marekani inataka kujenga ulimwengu wa kambi moja, lakini sasa historia itasajili  Afghanistan ya pili kwa Marekani huko Ukraine.

Mnamo Oktoba 2001, Marekani na washirika wake walianza kuingilia kijeshi nchini Afghanistan na kuikalia kwa mabavu nchi hiyo baada ya mashambulizi ya Septemba 11.

Baada ya miaka 20 ya vita nchini Afghanistan, Marekani iliondoa askari wake wa mwisho kutoka Afghanistan kwa madhila na unyonge mnamo Agosti 31, 2021.

Baada ya kuondoka wanajeshi wa Marekani kutoka Afghanistan, utawala wa nchi hiyo ilianguka mikononi mwa kundi la Taliban. Utawala wa rais wa sasa wa Marekani, Joe Biden na wa mtangulizi wake, Donald Trump zinalaumiwa kwa jinsi Washington ilivyoondoka Kabul kwa madhila baada ya kutumia matrilioni ya dola na kupoteza maelfu ya askari wake nchini Afghanistan bila ya faida yoyote.

Tags