Nov 30, 2023 02:30 UTC
  • Kuendelea siasa za chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya; kupigwa marufuku hijabu kazini

Ikiwa ni katika muendelezo wa siasa za chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi, marejeo ya juu zaidi ya kushughulikia sheria za Umoja wa Ulaya imetoa uamuzi wa kupiga marufuku vazi la hijabu kwa wafanyakazi katika nchi wanachama wa umoja huo.

Mahakama ya Ulaya, kikiwa ni chombo cha juu zaidi cha sheria katika Umoja wa Ulaya, imeamua kwamba wanachama wa EU wanaweza kuwazuia wafanyakazi kuvaa mavazi ambayo yanaashiria nembo na imani za kidini. Uamuzi huo umechukuliwa baada ya mwanamke mmoja nchini Ubelgiji kudai kwamba mwajiri wake alikiuka uhuru wake wa kidini kwa kumzuia kuvaa hijabu kazini.

Ingawa chuki dhidi ya Uislamu imeongezeka katika nchi za Ulaya katika miaka ya hivi karibuni, ambapo nyingi ya nchi hizo, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, zimekuwa zikidhulumu na kuwashinbikiza Waislamu, ambapo wanawake wamekuwa wakishinikizwa, kutukanwa, kunyanyaswa na kuvunjiwa keshima, lakini vitendo hivyo vya kibaguzi vimechukua sura mpya katika miezi ya hivi karibuni.

Katika miezi ya karibuni, nchi za Magharibi kwa kutunga sheria mbalimbali zilizo dhidi ya Uislamu zimetangaza rasmi siasa zao katika uwanja huo. Katika muktadha huo, tunaweza kutaja kupitishwa sheria inayokataza wasichana wa Kiislamu kuvaa hijabu katika shule nchini Ufaransa na kuruhusa kuchomwa Qur'ani Tukufu nchini Uswisi kuwa baadhi ya sheria hizo zinazolenga kubagua na kuwakandamiza Waislamu.

Nchi za Ulaya zinaeneza na kushadidisha siasa zilizo dhidi ya Uislamu, wakati ambapo zimekuwa zikidai kuheshimu uhuru na imani za dini tofauti kwa miongo kadhaa, na katika hali nyingi zimekuwa zikilaani nchi zingine kwa kisingizio cha kukiuka uhuru na kutoheshimu haki za binadamu.

Vazi la hijabu ni moja ya masuala muhimu yanayohadiliwa katika nchi za Magharibi. Nchi hizo kwa visingizio mbalimbali kama vile kudai kuwa hijabu ni kinyume cha sheria za usekula zinajaribu kuzuia rasmi hijabu na nembo za dini ya Kiislamu katika mfumo wa jamii ya Umoja wa Ulaya. Moja ya masuala muhimu katika nchi za Magharibi ni suala la hijabu na vazi la stara. Ripoti zinaonyesha kuwa nchini Ufaransa siasa za kibaguzi na chuki dhidi ya Waislamu hususan wanawake wa Kiislamu wanaovaa hijabu, zimeenea sana.

Katika nchi nyingine za Ulaya, hali ni hiyo hiyo, kwani bunge la Shirikisho la Ujerumani lilipitisha karibuni sheria inayopiga marufuku uvaaji wa alama za kidini kwa wafanyakazi wa serikali. Nchini Hungari, uchunguzi waliofanyiwa wanawake wa Kiislamu umeonyesha kuwa matusi yameongezeka sana dhidi yao na vilevile chuki dhidi ya wale wanaotuhumiwa kuwa ni wageni nchini humo. Hali hii imekuwa mbaya kwa kadiri  kwamba Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema siku chache zilizopita kwamba: Uhusiano kati ya chuki dhidi ya Waislamu na ukosefu wa usawa wa kijinsia hauwezi kukanushwa. Tunaona baadhi ya athari mbaya zaidi katika ubaguzi wa pande tatu dhidi ya wanawake wa Kiislamu kwa sababu ya jinsia, kabila na imani zao.

Maandamo ya kupinga sheria dhidi ya hijabu

Hivi sasa pia Mahakama ya Ulaya imechukua hatua nyingine katika siasa zake zilizo dhidi ya Uislamu kwa lengo la kuwashinikiza Waislamu. Hii ni katika hali ambayo kifungu cha 9 cha Hati ya Haki za Binadamu ya Ulaya kinasema: Kila mtu ana haki ya uhuru wa kujieleza, kimawazo, kifikra na kidini. Haki hii ni pamoja na uhuru wa kusema kuchagua dini, imani, kuabudu, kujifunza au kufuata mafundisho ya dini yoyote. Mahakama hiyo imeruhusu  kivitendo nchi za Ulaya kuwanyima wanawake uhuru wao wa kuchagua hijabu na hivyo kuhatarisha nafasi zao za kazi.

Taasisi za kisheria za nchi za Magharibi, zinahalalisha na kutoa tafsiri tofauti za kuwabana Waislamu, hasa wanawake wanaojisitiri kwa vazi la hijabu, katika hali hijabu si tu ni alama ya kidini, bali ni sehemu ya msingi ya utambulisho halisi wa wanawake wa Kiislamu, suala ambalo hupelekea wanawake wa Kiislamu kupoteza kazi na hadhi zao za kijamii.

Burhan Kasiji, Mkuu wa Baraza la Kiislamu la Ujerumani anasema: Tunataraji viongozi watawalinda Waislamu.

 

Tags