Feb 23, 2024 11:36 UTC
  • Dani Alves ahukumiwa kifungo cha miaka minne na nusu jela kwa ubakaji

Mbrazil Dani Alves, nyota wa zamani wa Barcelona na PSG, amehukumiwa na mahakama ya Barcelona kifungo cha miaka minne na nusu jela kwa kosa la kumbaka msichana katika klabu ya usiku jijini humo Desemba 2022.

Kuna ushahidi ambao, zaidi ya ushuhuda wa mlalamishi, unawezesha ubakaji kuchukuliwa kuwa umethibitishwa," mahakama imesema katika taarifa.

Alves, ambaye amekuwa kizuizini kabla ya kesi hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja na atakata rufaa dhidi ya uamuzi huu, kwa mujibu wa wakili wake, pia ameagizwa kulipa euro 150,000 kwa msichana huyo na kukaa mbali naye kwa miaka tisa na nusu, pamoja na miaka mitano ya kuachiliwa kwa kufuatiliwa mara baada ya kifungo chake kutekelezwa.

 

Katika uamuzi wake, mahakama iliangazia vidonda kwenye magoti ya mwathiriwa, na kuvielezea kama "matokeo ya vurugu iliyosababishwa na Alvès".

Aidha Mahakama imesema kuwa ushahidi wa mwathiriwa umekuwa "sawa" wakati wote wa utaratibu na kwamba hakuwahi kutaka kupata "maslahi ya kiuchumi" kutokana na jambo hili.

Hukumu ya Alves, 40, mwishoni mwa kesi hii iliyotangazwa sana, ambayo ilifanyika mapema Februari, ilizua hisia hata kutoka kwa serikali ya mrengo wa kushoto ya Uhispania, ambayo ilipitisha sheria yenye utata juu ya idhini mnamo 2022 ya ngono ya wazi.

Tags