Al Azhar, Misri yalaani mauaji ya kigaidi ya Nice
Chuo Kikuu cha al Azhar nchini Misri kimetoa taarifa na kutaka kuwepo umoja na mshikamano duniani ili kukabiliana na ugaidi.
Al Azhar imelaani shambulizo la jana usiku katika mji wa Nice Ufaransa lililosababisha vifo vya watu zaidi ya 80 na kuzitolea wito nchi zote kuwa kitu ili kuendesha mapambano dhidi ya ugaidi.
Taarifa ya Chuo al Azhar pia imesema kuwa shambulio hilo la kigaidi linakinzana na mafundisho ya Uislamu na kusisitzia udharura wa kuunganisha juhudi kimataifa ili kuutokomeza ugaidi.
Rais Francois Hollande wa Ufaransa amelitaja shambulio hilo kuwa la kigaidi na amerefusha muda wa hatari nchini humo kwa miezi mingine mitatu. Kundi la kigaidi la Daesh limetangaza kuhusika na shambulio hilo ambalo linaendelea kulaaniwa na jumuiya na taasisi mbalimbali kote duniani.