Waungaji mkono wa Palestina wakatiza hotuba ya Harris
(last modified Thu, 31 Oct 2024 02:36:37 GMT )
Oct 31, 2024 02:36 UTC
  • Waungaji mkono wa Palestina wakatiza hotuba ya Harris

Waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina wamekatiza hotuba ya Makamu wa Rais wa Marekani na mgombea wa chama cha Democratic, Kamala Harris wakati wa mkutano wake wa kampeni za uchaguzi wa rais huko Washington DC.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, Kamala Harris akiwa katika mkatano wa kampeni mjini Washington, DC alikabiliwa na maandamano kutoka kwa mamia ya watu walioonyesha kutoridhishwa na sera ya utawala wa mwanasiasa pamoja Rais Joe Biden kuhusu Gaza.

Ikiwa imesalia chini ya wiki moja tu kabla ya uchaguzi wa rais wa Marekani wa Novemba 5, Harris alifanya mkutano kwenye Ellipse katika mji mkuu, eneo lile lile ambapo Rais wa zamani Donald Trump alihutubia wafuasi wake kabla ya shambulio la Januari 6, 2021 Capitol. 

Alipokuwa akihutubia umati wa watu, waandamanaji zaidi ya 300 walianza kupiga nara za kukosoa sera za utawala wa Biden na Harris kuhusu Gaza, wakivuta hisia za idadi kubwa ya Wamarekani.

Waandamanaji hao walikuwa wamebeba mabango yenye jumbe za kutaka Israel iwekewe vikwazo vya silaha, huku wakisisika wakiimba “Kamala, unasemaje? Hatutakupigia kura siku ya uchaguzi. Umeua watoto wangapi (wauawa) leo (Gaza)?"

Makundi ya kisiasa, kidini na kijamii nchini Marekani yamekuwa yakimshinikiza Rais Joe Biden wa nchi hiyo alaani vitendo vya ugaidi wa kiserikali vinavyofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.

 

Tags