Padri nchini Indonesia anusurika kuuawa na mwanachama wa Daesh
https://parstoday.ir/sw/news/world-i14197-padri_nchini_indonesia_anusurika_kuuawa_na_mwanachama_wa_daesh
Polisi ya Indonesia imetangaza habari ya kunusurika kuuawa padri mmoja wa nchi hiyo kutokana na hujuma ya mwanachama wa kundi la kigaidi la Daesh (ISIS).
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 29, 2016 09:26 UTC
  • Padri nchini Indonesia anusurika kuuawa na mwanachama wa Daesh

Polisi ya Indonesia imetangaza habari ya kunusurika kuuawa padri mmoja wa nchi hiyo kutokana na hujuma ya mwanachama wa kundi la kigaidi la Daesh (ISIS).

Kwa mujibu wa ripoti, Alberto Pandyangan kiongozi wa kanisa lililoko katika mji wa Medan, alinusurika kuuawa kwa shoka na kisu hapo jana. Habari zaidi zinasema kuwa, mkono wa padri huyo mwenye umri wa miaka 60 ulijeruhiwa katika hujuma hiyo. Kadhalika polisi ya Indonesia imetangaza kuwa, gaidi huyo mwenye umri wa miaka 18 kwa jina la Ivan Armadi Hasugian aliingia kanisani majira ya asubuhi pamoja na watu wengine na kukaa miongoni mwa waumini. Muda punde baadaye alilipua bomu la kutengeneza kwa mkono hata hivyo bomu hilo halikuwa na athari ambapo liliishia kumjeruhi yeye mwenyewe.

Msemaji wa jeshi la polisi mjini Sumatera, Rina Sari Ginting, amesema kuwa baada ya hapo gaidi huyo alisimama na shoka na kisu mkononi mwake kumwendea padri ambapo alimjeruhi mkono. Hata hivyo waumini walimvamia haraka na kumkabidhi kwa polisi. Kwa mujibu wa polisi, kijana huyo alipatikana na kitambulisho kilichoandikwa jina la Ivan Armadi Hasugian na kadhalika karatasi iliyokuwa na alama za kundi la Daesh.