Rais Putin: Marekani imetumbukia katika shimo lile lile
https://parstoday.ir/sw/news/world-i18355-rais_putin_marekani_imetumbukia_katika_shimo_lile_lile
Rais Vladimir Putin wa Russia ameelezea kusikitishwa kwake na makubaliano yaliyofikiwa kati ya nchi yake na Marekani katika suala la kupambana na ugaidi lakini hayakutekelezwa kivitendo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 28, 2016 23:09 UTC
  • Rais Putin: Marekani imetumbukia katika shimo lile lile

Rais Vladimir Putin wa Russia ameelezea kusikitishwa kwake na makubaliano yaliyofikiwa kati ya nchi yake na Marekani katika suala la kupambana na ugaidi lakini hayakutekelezwa kivitendo.

Rais wa Russia ameikosoa vikali Marekani na kusema kuwa, kwa mara nyingine imetumbukia katika shimo lile lile ililotumbukia ndani huko nyuma. Rais wa Russia amesema kuwa, inasikitisha kuwa, makubaliano ya Moscow na Washington katika uwanja wa kupambana na ugaidi hayajatekelezwa kivitendo na kuongeza kama ninavyomnukuu: Hata makubaliano yetu ya faragha na Rais wa Marekani hayajasaidia chochote."

Ameongeza kuwa, kuna watu huko Washington wamesimama na kufanya kila wawezalo kuhakikisha kwamba, makubaliano yaliyofikiwa kati ya Russia na Marekani kuhusiana na suala zima la kupambana na ugaidi hayatekelezwi kivitendo.

Marais Vladimir Putin wa Russia na Barack Obama wa Marekani

Rais Putin amesema kuwa, mbinu hii ni ya ajabu na isiyo na hekima ambayo kwa hakika inaonyesha hamu ya madola ya Magharibi ya kukaririwa makosa ya huko nyuma, au kama ilivyo mashuhuri: Inaonekana kuwa madola hayo yanataka kutumbukia katika shimo lile lile yaliyotumbukia hapo kabla. 

Hayo yanajiri siku chache tu, baada ya Rais Putin kusisitiza kwamba, hakuna mazungumzo yatakayofanyika baina ya Miscow na Washington katika kipindi cha sasa.

Putin alisema mazungumzo katika mtazamo wa Marekani ni kwamba nchi hiyo huwasilisha matakwa yake kwenye meza na kisha kushinikiza yatekelezwe na kuongeza kuwa, mbinu inayotumiwa na Marekani si mazungumzo, bali ni njia ya kutaka kuzitwisha nchi nyingine matakwa yake.