Nov 21, 2016 07:19 UTC
  • Putin amuunga mkono Trump kuhusiana na ustawi wa biashara

Rais Vladimir Putin wa Russia amesisitiza kuwa Donald Trump, rais mteule wa Marekani hatavuruga masuala yanayohusiana na ustawishaji wa biashara katika eneo la Bahari ya Pacific.

Shirika la habari la Sporting limemnukuu Rais Putin aliyekuwa akizungumza jana Jumapili mwishoni mwa kikao cha viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Bahari ya Pacific APEC huko Lima mji mkuu wa Peru akisema kwamba kuchaguliwa Trump kuwa rais wa Marekani hakutatoa pigo kwa mwenendo wa kustiwisha biashara katika eneo la Bahari ya Pacific.

Putin vilevile amesisitiza kwamba Trump amemwambia kuwa ana lengo la kuimarisha tena uhusiano  ulioharibika kati ya nchi yake na Russia kutokana na masuala yanayohusiana na Ukraine na Syria. Putin ameongeza kuwa kwa kawaida katika kila nchi kuna tofauti kubwa kati ya nara zinazopigwa wakati wa kufanyika kampeni za uchaguzi na siasa halisi za nchi hizo.

Rais Putin akizungumza na Rais Obama wa Marekani

Putin ameongeza kuwa katika kipindi cha uongozi wa Rais Barack Obama wa Marekani serikali ya Moscow ilifanya juhudi kubwa za kuimarisha uhusiano na serikali ya Washington lakini kwamba kufanya kazi na rais huyo lilikuwa suala gumu.

Putin na Obama walikutana jana kwa kipindi kifupi huko Lima ambapo walijadili kwa ufupi masuala muhimu ya kimataifa, ikiwemo migogoro ya Ukrain na Syria.

Tags