Waingereza wenye asili ya Afrika wanabaguliwa katika kazi za uhandisi
(last modified Wed, 28 Dec 2016 02:50:00 GMT )
Dec 28, 2016 02:50 UTC
  • Waingereza wenye asili ya Afrika wanabaguliwa katika kazi za uhandisi

Waingereza weusi au wenye asili ya Afrika wanakabiliwa na ubaguzi katika ajira ambapo wengi wananyimwa kazi kutokana na rangi yao.

Taarifa ya gazeti la Guardian imesema kuwa, Waingereza weusi ambao wamehitimu katika taaluma ya uhandisi Uingereza wakilinganishwa na wenzao wazungu, wana  fursa ndogo sana ya kupata kazi za uhandisi.

Ripoti hiyo imesema Waingereza weusi ambao ni katika kaumu za waliowachache wanakabiliwa na ubaguzi katika masomo, mikopo ya masomo na wanaohitimu wanabaguliwa katika soko la ajira.

Maandamano ya kuteteua haki za watu weusi katika nchi za Magharibi

Ripoti ya Guardian imeonyesha kuwa asilimia 71 ya wazungu wanaohitimu katika taaluma ya uhandisi katika miezi sita iliyopita walipata kazi kamili hata kabla ya kuondoka kwenye vyuo vikuu. Katika upande mwingine asilimia 52 ya Waingereza wenye asili ya Asia wanapata kazi huku Waingereza wenye asilia ya Afrika wakiwa ni asilimia 46.

Takwimu hizi zinaonyesha kuwepo ubaguzi wa wazi katika serikali ya Uingereza ambayo inadai kutetea haki za binaadamu. Ubaguzi huo wa Waingereza weusi wahandisi unajiri wakati ambao Uingereza inadai kuna uhaba wa wahandisi kitaifa.