Iran yalaani hujuma ya kigaidi nchini Russia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i27242-iran_yalaani_hujuma_ya_kigaidi_nchini_russia
Jamhuri ya Kiislamu ya Kiislamu ya Iran imelaani hujuma ya kigaidi katika mji wa St.Petersburg nchini Russia.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Apr 03, 2017 22:58 UTC
  • Iran yalaani hujuma ya kigaidi nchini Russia

Jamhuri ya Kiislamu ya Kiislamu ya Iran imelaani hujuma ya kigaidi katika mji wa St.Petersburg nchini Russia.

Katika taarifa, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bahram Qassemi ametuma salamu za rambirambi kwa serikali na taifa la Russia kufuatia tukio hilo la kigaidi.

Ameongeza kuwa, mauaji ya raia wasio na hatia kwa lengo lolote lile ni jambo linalolaaniwa vikali. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu inasisitiza kuhusu kushirikishwa jamii ya kimataifa katika vita vya kweli dhidi ya ugaidi. Amesema azma na irada ya serikali zote na mashirika ya kimataifa ni dharura katika kung'oa mizizi ya ugaidi duniani.

Mlipuko wa Bomu katika treni ya chini ya ardhi (Metro) mjini St. Petersburg Russia

Jana Jumatatu watu 11walipoteza maisha na wengine 45 kujeruhiwa katika mripuko uliotokea ndani ya treni ya chini ya ardhi (Metro) mjini Saint Petersburg. Rais Vladimir Putin wa Russia amesema uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea. Mlipuko huo umejiri wakati rais Putin akiwa safarini katika mji huo wa bandarini.