Waislamu 21 wauawa Myanmar katika mapigano jimboni Rakhine
https://parstoday.ir/sw/news/world-i33600-waislamu_21_wauawa_myanmar_katika_mapigano_jimboni_rakhine
Waislamu 21 wameuawa katika mapigano yaliyozuka usiku wa kuamkia leo nchini Myanmar katika jimbo la Rakhine la magharibi mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 25, 2017 07:43 UTC
  • Waislamu 21 wauawa Myanmar katika mapigano jimboni Rakhine

Waislamu 21 wameuawa katika mapigano yaliyozuka usiku wa kuamkia leo nchini Myanmar katika jimbo la Rakhine la magharibi mwa nchi hiyo.

Taarifa zinasema kuwa, maafisa watano wa polisi pia wameuawa katika mapigano hayo yaliyotokea kwenye jimbo hilo lenye Waislamu wengi ambao wamekuwa wakikandamizwa kwa miongo kadhaa sasa.

Taarifa ya serikali ya Myanmar imedai kuwa wanamgambo, iliowataja kuwa  kuwa Wabengali, walishambulia vituo 24 vya polisi na kwamba kulikuwa na watu 150 waliojaribu kuvamia kambi ya jeshi. Hata hivyo Waislamu wa Myanmar hawajasema chochote hadi hivi sasa kuhusu madai hayo ya serikali ya nchi hiyo.

Serikali ya Myanmar ya Myanmar inadai kuwa Waislamu wa Rohingya wamapatao milioni 1.1 ni Wabengali ikimaanisha ni wenyeji wa Wabangladesh na hivyo kuwanyima haki yao ya uraia.

Mabuddha wenye misimamo mikali wanaowaangamiza Waislamu Myanmar

Mapema mwezi huu Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imeitaka serikali ya Myanmar kuheshimu haki za Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini humo ambao wanakandamizwa na serikali na kuhujumiwa na Mabuddha wenye misimamo mikali.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa Waislamu wa kabila la Rohingya ni jamii ya wachache inayodhulumiwa na kunyongeshwa zaidi duniani. 

Katika miaka ya karibuni, Waislamu wengi wa kabila la Rohingya nchini Myamnar wameuawa au kulazimika kuhama makazi yao na kuwa wakimbizi katika nchi za Bangladesh, Thailand, Malaysia na Indonesia kutokana na mashambulio ya Mabuddha wenye misimamo ya kufurutu mpaka wanaoungwa mkono na serikali ya nchi hiyo.