Russia yaonya itakabiliana na chokochoko za Marekani Syria
https://parstoday.ir/sw/news/world-i42922-russia_yaonya_itakabiliana_na_chokochoko_za_marekani_syria
Mbunge wa ngazi za juu nchini Russia ameionya Marekani isichukue hatua zozote zilizo kinyume cha sheria nchini Syria kufuatia madai ya hivi karibuni ya kujiri hujuma ya silaha za kemikali katika mji unaoshikiliwa na magaidi wa Douma.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 10, 2018 12:18 UTC
  • Russia yaonya itakabiliana na chokochoko za Marekani Syria

Mbunge wa ngazi za juu nchini Russia ameionya Marekani isichukue hatua zozote zilizo kinyume cha sheria nchini Syria kufuatia madai ya hivi karibuni ya kujiri hujuma ya silaha za kemikali katika mji unaoshikiliwa na magaidi wa Douma.

Vladimir Shamano, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi katika Bunge la Russia, Douma, ambaye pia aliwahi kuwa kamanda wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Russia amesema, 'sera za undumakuwili zimefika ukingoni. Na hapa, Chama cha Russia Moja, kinasisitza kuwa hatua zote za kisiasa, kidiplomasia na kijeshi zitachukuliwa. Hatua zote zilizo kinyume cha sheria zitakabiliwa na jibu."  Aidha amesema ripoti za kuwepo hujuma ya kemikali mjini Douma ni 'uchochezi kamili'.

Hii ni katika hali ambayo madola ya Maghaibi yameendelea kutoa tuhuma dhidi ya serikali ya Rais Bashar al-Assad wa Syria kuhusiana na kadhia ya shambulizi hewa la silaha za kemikali katika mji wa Douma, ambapo katika uwanja huo imeelezwa kuwa kongresi ya Marekani inafanya njama za kumshawishi Rais Donald Trump kufanya shambulizi dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Bunge la Russia

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria pia imetangaza kuwa, tuhuma za uongo za baadhi ya nchi dhidi ya serikali ya Damascus kuhusiana na silaha za kemikali, zinalenga kuendeleza uhai wa makundi ya kigaidi nchini Syria. Kufuatia madai hayo, vyombo vya habari vya nchi za Magharibi na vinavyoyaunga mkono makundi ya kigaidi, vimeanzisha vita vya kisaikolojia dhidi ya serikali ya Syria. Inafaa kuashiria kuwa, hadi sasa makundi ya kigaidi na ya Kiwahabi yameshafanya jinai nyingi nchini Syria, ikiwemo ya kutumia silaha za kemikali dhidi ya raia.