Mashirika ya bima yapinga kupatiwa silaha za moto walimu nchini Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i45062-mashirika_ya_bima_yapinga_kupatiwa_silaha_za_moto_walimu_nchini_marekani
Gazeti la Washington Post limeandika kuwa, mashirika ya bima nchini Marekani yamepinga pendekezo la kupatiwa silaha za moto walimu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 27, 2018 23:46 UTC
  • Mashirika ya bima yapinga kupatiwa silaha za moto walimu nchini Marekani

Gazeti la Washington Post limeandika kuwa, mashirika ya bima nchini Marekani yamepinga pendekezo la kupatiwa silaha za moto walimu.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, hadi sasa mashirika ya bima katika jimbo la Kansas bado yanaendelea kupinga suala la kupatiwa walimu wa shule za umma silaha hizo. Linafafanua kuwa, licha ya jimbo la Kansas kuruhusu suala la walimu hao kubeba silaha wanapokuwa darasani, lakini hadi sasa hakuna shule hata moja ambayo imetii sheria hiyo.

Mmoja wa wanafunzi waliowahi kutekeleza mashambulizi shuleni na kusababisha maafa

Shirika la EMC ambalo ni shirika kubwa la bima kwa ajili ya shule za jimbo hilo limetoa ujumbe kwa wanachama wake kwamba limefikia natija kuwa, kubeba silaha za moto mashuleni kunaongeza majukumu yake. Kuongezeka vitendo vya mashambulizi ya silaha za moto katika shule nchini Marekani, kumeibua mgogoro hata kwa mashirika ya bima ya nchi hiyo. Rais Donald Trump wa nchi hiyo na viongozi wa mrengo wa kulia wanaunga mkono suala la walimu kubeba silaha mashuleni. Hata hivyo msimamo huo, umekabiliwa na upinzani mkubwa wa pande nyingine husika nchini humo.